Sijawahi kujaribu kuomba msamaha WCB - Rich Mavoko
Msanii wa Bongo Fleva, Rich Mavoko amesema alishtushwa na taarifa zilizokuwa zinasambaa mtandaoni kuwa ameomba msamaha ili arudi kufanya kazi na lebo ya WCB.
Akizungumzia ishu hiyo, Mavoko ambaye alijitoka WCB mwaka jana, alisema alisikia taarifa hizo za kizushi kupitia mdogo wake lakini baada ya kufuatilia aligundua ni uongo hivyo akapuuzia.
"Sijawahi kujaribu kuomba msamaha na hakiwezi kutokea kitu kama hicho, bora nivae shati lililochanika kuliko kutembea tumbo wazi, kikubwa naomba mashabiki zangu waendelee kunipa sapoti kupitia wimbo wangu mpya Usizuge,” Mavoko ameimbia Clouds FM.
Kwa sasa Rich Mavoko anafanya vizuri na wimbo wake unaokwenda kwa jina la Usizuge kutoka chini la lebo ya Bilionea Kid.
Comments
Post a Comment