Waamuzi atakaocheza fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC)

Nahodha wa Lipuli FC Ally Mtoni (Kulia) na Agrey Moris wa Azam FC (Kushoto) wakitakiana mchezo wa Kiungwana kuelekea Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) itakayochezwa Kesho Jumamosi Juni 1,2019 Uwanja wa Ilulu,Lindi

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limemtangaza Hance Mabena (pichani) kutoka Tanga kuwa mwamuzi wa mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) utakaopigwa kesho Juni 01, 2019. .

Katika mchezo huo watatumika waamuzi sita kwa mara ya kwanza kwenye historia ya soka la Tanzania ambapo Mabena atasaidiwa na jumla ya waamuzi watano (wawili wa pembeni , wawili wa kwenye magoli na mwamuzi mmoja wa akiba). .

Mfumo wa kuwa na waamuzi sita ulianza kutumiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwenye AFCON ya vijana chini ya miaka 17 iliyofanyika nchini mwezi Aprili 2019.

Kwa mujibu wa taarifa ya TFF iliyotolewa leo, Hance Mabena atasaidiwa na Mohamed Mkono kutoka Tanga kama mwamuzi msaidizi namba moja, Frednarnd Chacha kutoka Mwanza kama mwamuzi msaidizi namba 2, na Abubakar Mturo kutoka Mtwara atakuwa ni mwamuzi wa akiba.

Waamuzi wasaidizi walioteuliwa kukaa kwenye magoli ni Martin Sanya kutoka Morogoro na Florentina Zablon kutoka Dodoma huku mtathmini wa waamuzi akiwa ni Lesile Liunda kutoka Dar es Salaam na kamishna wa mchezo ni Salum Kurunge kutoka Geita.




Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato