R. Kelly aongezewa mashitaka mengine 11
R.Kelly ameshtakiwa kwa makosa 11 ya unyanyasaji wa kingono, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini Marekani.
Mahakama imeripotiwa kuonyesha kuwa vitendo hivyo vilifanywa dhidi ya watoto wa umri kati ya miaka 13 na 16, na ikiwa itathibitika atakabiliwa na adhabu kali kuliko adhabu nyingine anazokabiliwa nazo.
Mwanzoni mwa mwaka huu msanii huyo wa miondoko ya R&B alikabiliwa na mashtaka 10 ya unyanyasaji wa kingono. Alikana kuhusuka na vitendo hivyo na akaachiwa huru kwa dhamana.
Ikiwa atakutwa na hatia kwa mashtaka ya awali, yaliyohusisha wanaodaiwa kuwa waathirika wa vitendo hivyo, wakiwemo wasichana wadogo watatu,atakabiliwa na kifungo cha miaka mitatu mpaka saba gerezani.
Wakili wa R.Kelly Steve Greenberg amesema mashtaka ya sasa si kwamba ni kesi mpya.
''Ameshtakiwa kwenye kesi ambayo bado ipo, ikihusisha watu walewale wanaodaiwa kuwa waathirika na muda uleule (miaka 10 iliyopita) hakijabadilika kitu'', aliandika kwenye ukurasa wa Twitter.
''Mashtaka ni yale yale ni kwamba tu yametolewa kwa nyakati tofauti, wadai ni walewale, muda ni ule ule, ushahidi ni uleule.Tunatarajia matokeo yaleyale.''
Mwandishi wa Chicago Tribune Megan Crepeau ameripoti kuwa mashtaka mapya manne dhidi yake ni makubwa sana kuwahi kutokea katika jimbo la Illinois, ambayo adhabu yake ni kifungo cha miaka 6 mpaka 30.
Mwanzoni mwa mwaka huu msanii huyo wa miondoko ya R&B alikabiliwa na mashtaka 10 ya unyanyasaji wa kingono. Alikana kuhusuka na vitendo hivyo na akaachiwa huru kwa dhamana.
Comments
Post a Comment