Rais Ramaphosa wa Afrika Kusini achagua Baraza la Mawaziri
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amechagua Baraza jipya la Mawaziri, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupambana na rushwa iliyotawala katika serikali yake.
Ramaphosa ameonya kwamba mawaziri hao watafuatiliwa kwa karibu, Baraza hilo jipya lina mawaziri 28 badala ya 36 wa baraza lilopita na nusu yake ni wanawake.
Ramaphosa amechagua mawaziri wake kutoka ndani na nje ya chama chake cha African National Congress (ANC).
Matarajio ni makubwa miongoni mwa wanachi wa Afrika Kusini, waliokichagua tena chama cha ANC katika uchaguzi wa Mei 8.
Wanamtegemea Ramaphosa kuleta mfumo mpya wa uongozi baada ya taifa hilo kwa miaka kadhaa kukabiliwa na kashfa tofauti.
Kuteuliwa tena kwa David Mabuza kama Naibu Rais kumezua malalamiko kutoka upande wa upinzani. Jina la Mabuza limehusishwa na rushwa na tume ya uadilifu ya chama cha ANC.
Comments
Post a Comment