Waziri Mkuu afurahishwa na ujenzi uwanja wa ndege Julius Nyerere
Waziri Mkuu amesema kuwa amefurahishwa na kukuta michoro ya wanyama kama tembo, twiga, bahari, minazi na majahazi ambayo ni alama za nchi.
Mradi wa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika Mei 30, mwaka huu ambapo hadi sasa tayari maeneo mengi yamekamilika ikiwa ni pamoja na sehemu za abiria wanaowasili na kuondoka.
Kufuatia kukamilika kwa uwanja huo kwa asilimia 95, Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ianze kukamilisha taratibu za kuutumia uwanja huo ili mkandarasi anapoukabidhi uanze kutumika.
Comments
Post a Comment