Mwili wa Ruge Mutahaba kuwasili nchini leo
Taarifa kwa Umma.
Mwili wa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba utawasili leo saa 9:00 Alasiri kutoka South Africa.
Hii ni Ramani ya njia rasmi mwili utakapopita hadi kufikishwa hadi Hospital ya Lugalo kupumzishwa. Wakazi wa jiji la Dar es Salaam na maeneo ya jirani wametangaziwa kujipanga pembezoni mwa Barabara wakati mwili wa Ruge ukipita kwa heshima za mwisho.
Route yake itakuwa hivi: Airport - Buguruni - Barabara ya Uhuru - Karume - Magomeni - Morocco Hotel - Sinza Kijiweni - Bamaga - ITV - Clouds - Kawe - Lugalo.
Ruge Mutahaba atakwenda kuzikwa nyumbani kwao huko Bukoba siku ya Jumatatu, siku ya Jumapili mwili utasafirishwa kwenda Bukoba.
Ruge Mutahaba amefariki siku ya February26 mwaka huu nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu ya figo. Ruge alizaliwa mwaka 1970, Brooklyn nchini Marekani, atakumbukwa zaidi kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya muziki nchini.
Comments
Post a Comment