Mtazamo chanya bila kuwa na kitu hiki ni sawa na bure


Inasemekana ya kwamba mtazamo chanya ni rasilimali tosha dhidi ya kuuaga umaskini, aidha watalamu wa masuala haya ya elimu ya mafanikio wanazidi kusisitiza ya kwamba ili mtu aweze kufanikiwa anatakiwa kuibeba mitazamo  hiyo chanya kila wakati.

Lakini licha ya watu wengi kuibeba mitazamo hiyo chanya wamekuwa wakisahau kitu kimoja, kitu  hicho  ni muhimu sana kwani huenda sambamba na mitazamo hiyo chanya. Na leo nataka nikwambie kitu hicho, kwani kuwa na mtazamo chanya bila ya kuwa na kitu hicho ni sawa na bure.

Kitu chenye ni hiki, mtazamo chanya huenda sambamba na " kuwajibika" watu wengi kama ujuzi  na maarifa wanayo ya kutosha, ila tatizo ni kule kunakowafanya watu hao kuwa mtazamo chanya zaidi ila wamesahau kuwajibika juu ya kitu walichonacho.

Tangu umeanza kujifunza mambo mbalimbali ya mafanikio naamini mpaka sasa kwa sehemu fulani una mtazamo chanya juu ya jambo fulani, ila kinachokoseana kutoka kwako ni kule kunakoitwa kuwajibika juu ya mtazamo huo.

Hivyo mimi naamini kutokufanikiwa kwako kimaisha umeamua mwenyewe, nasema hivi kwa sababu hutaki kuchua hatua kwa ile hali uliyonayo, wengi huamaini mafanikio huja kesho, lakini kadri siku sinavyozidi kwenda hujikuta maisha yao yapo vilevile na hiyo kesho yao isiyokuwa na mipaka.

Kama wewe ni miongoni mwa watu wanaosema nitafanya kesho, nakusihi ya kwamba achana na dhana hiyo kwani mafanikio ya kesho hutengenezwa na leo, pia amini kwamba binadamu huishi siku moja, siku hiyo leo, kesho si rafiki kwako.

Hivyo kwa kile kidogo ulichonacho matharani mtazamo chanya ulionao ni nguzo sahihi ya mafanikio yako endapo utaamua kuwajibika juu ya jambo hilo unalolifahamu. Kuchukua hatua ni sehemu kubwa ambayo itakutoa hapo ulipo kwenda sehemu nyingine ya mafanikio.

Na. Benson Chonya.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato