Simba SC kuwafuata Stand United leo
Kikosi cha Simba SC kinaondoka leo mjini Singida kuelekea Shinyanga ambako siku ya Jumapili
watacheza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stand United.
Hapo jana jioni Wachezaji wa kikosi hicho walifanya mazoezi kwenye uwanja wa Namfua ili
kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo huo.
Hadi sasa Simba SC wamecheza michezo 19 ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL) na kujikusanyia pointi 48, wakati Yanga Sc na Azam FC waliowatangulia wekundu hao wakiwa wamecheza michezo 25 kwa kila mmoja.
Comments
Post a Comment