Msanii Ariana Grande aongoza kwa wafuasi mtandao wa Instagram
Mwanamuziki wa Pop Ariana Grande amekuwa staa wa kike duniani mwenye idadi kubwa zaidi ya wafuasi (followers) kwenye mtandao wa Instagram, nafasi iliyokuwa inashikiliwa mwanzoni na Selena Gomez.
Ariana Grande amefikisha idadi ya wafuasi Millioni 146.3 huku SelenaGomez akiwa nyuma yake
kwa wafuasi Millioni 146.2.
Kwa miaka mitatu Selena alikuwa ameshikilia nafasi ya kwanza kwa mastaa wenye wafuasi wengi
zaidi duniani hadi cristiano Ronaldo alivyompindua Oktoba mwaka jana.
Kwasasa anayechezea klabu ya Juventus nchini Italy ndiye anaongoza akiwa na wafuasi wengi
zaidi kwenye mtandao huo akiwa na wafuasi millioni 155.9.
Comments
Post a Comment