NBS na Sheria mpya ya utoaji Takwimu
Ofisi ya Taifa ya Takwimu –NBS imetoa maelezo ya marekebisho ya Sheria ya Takwimu Namba 9 ya mwaka 2015 katika ofisi za takwimu zilizopo barabara ya Sokoine jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano, Mkurugenzi Mtendaji wa NBS, Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa sheria ya takwimu ya Mwaka 2015 imerekebishwa kupitia Sheria Namba 8 ya mwaka 2018.
Dkt Chuwa amesema “Lengo la marekebisho hayo, ni kuimarisha utaratibu wa usambazaji takwimu nchini, kwa nia ya kuepusha kutoa takwimu zinazokinzana kwa jamii, pia, marekebisho hayo yanalenga kuimarisha mijadala ya kisera pamoja na matokeo yake’.
Aidha, marekebisho ya sheria hiyo ambayo yamejikita zaidi katika kuweka utaratibu wa uchambuzi wa kina kutumia mfumo wa kuweka takwimu ‘Dataset’ zinazotokana na tafiti kadhaa ambazo nyingi zimewekwa kupitia kwenye tovuti ya NBS na baadhi zipo kwenye hifadhi zetu, amesema Dkt. Chuwa.
Akieleza utaratibu wa utoaji wa takwimu ambazo zitatofautiana na zilizotolewa awali na Ofisi ya takwimu amesema kuwa ambapo ikitokea kuna matokeo yaliyowekwa na tofauti na yale yaliyotolewa na NBS katika kiashiria cha aina hiyo, marekebisho yanaweka utaratibu wa namna bora ya utoaji ya matokeo hayo.
Pamoja na hayo Dkt. Chuwa amesema kuwa marekebisho yamelenga zaidi kuondoa mkanganyiko kwa jamii unaoweza kutokea iwapo zitatolewa takwimu zenye lengo la kupotosha takwimu zilizotolewa awali, takwimu za aina hii ni zile zimetolewa bila kufanyiwa utafiti wa kutosha,”
Kufuataia marekebisho hayo ya kitakwimu ya mwaka 2017 zimeanza kupitiwa ili kuwezesha utekelezaji wa marekebisho ya sheria ambapo kanuni zake zitatoa ufafanuzi wa namna bora ya utekelezaji wa matakwa ya kisheria.
Vilevile, Dkt Chuwa amesema “Marekebisho haya hayana lengo la kuingilia mchakato wa ukusanyaji wa takwimu ambazo zinakuswanya kwa matumizi ya ndani”.
Comments
Post a Comment