Simba kuvaana na Costal Union leo
Timu ya soka ya Simba kuoneshaana ubabe na Costal Union leo ambao mchezo utachezwa kwenye Uwanja wa Uhuru ukiwa ni mchezo wa ligi kuu. Simba kwa sasa wako nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 44 baada ya kucheza mechi 17, Coastal Union wenyewe wapo nafasi ya tatu na alama zao 30, wamecheza mechi 17 kama wapinzani wao. Sasa rekodi zinaonyesha kuwa kwa msimu uliopita wa 2018/19 ambao Coastal Union ilipanda daraja, iliambulia kichapo mechi zake zote mbele ya Simba jambo linaloufanya mchezo wa leo kuwa mgumu.