Shirika la afya duniani latangaza corona kuwa janga la dunia
Virusi vipya vya corona vimetangazwa kuwa janga la dharura,wakati virusi hivyo vikiendelea kusambaa kwa kasi nje ya China, kwa mujibu wa shirika la afya duniani(WHO).
"Sababu kubwa ya tangazo hilo si kwa sababu ya kile ambacho kinatokea China kwa sasa lakini kile ambacho kinatokea katika mataifa mengine," alisema kiongozi mkuu wa shirika la afya duniani Tedros Adhanom Ghebreyesus .
Kinachoangaziwa zaidi ni kuhusu ugonjwa huo kusambaa mataifa mengine huku kukiwa na mfumo duni wa afya
Shirika la afya duniani limesema kuwa kumekuwa na visa 98 katika mataifa mengine 18 ingawa hakuna vifo vilivyobainika. Visa vingi vya wagonjwa hao walikuwa wamesafiri kutoka mji wa Wuhan, eneo ambalo mlipuko wa ugonjwa huo ulianza.
Hata hivyo kuna kesi nane zilizosababishwa na maambukizi ya kati ya mtu kwa mtu huko Ujerumani, Japan, Vietnam na Marekani.
Akizungumza katika mkutano wa habari Geneva, Dkt Tedros alielezea virusi vya corona kuwa mlipuko wa ugonjwa ambao haujawahi kutokea awali na bado haujaweza kupata suluhu.
Dkt.Tedros alisifia hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na serikali ya China katika kuzuia maambukizi yasienee na alisema kuwa hakukuwa na sababu ya kuzuia watu wasisafiri au biashara zisiendelee.
Lakini nchi mbalimbali zimechukua hatua ya kufunga mipaka na kusitisha safari za ndege za nchini China, vivyo hivyo makampuni makubwa pia yamefunga maduka yao.
Comments
Post a Comment