Wataalamu wa kilimo cha umwagiliaji wajadiliana juu ya kuwajengea uwezo wakulima
Wataalam wa kilimo cha umwagiliaji wameendelea na majadiliano Jijini Dodoma huku, wakibadilishana mawazo na uzoefu kuhusiana na Mradi wa kuwajengea uwezo wakulima na wataalam katika Kilimo cha Umwagiliaji wakijikita zaidi katika shughuli za mradi huo,mafanikio na Changamoto na namna ya kutatua changamoto hizo ambazo zinaweza kupelekea Mradi huo kuwa endelevu hata baada ya muda wake kufikia mwisho.
Wataalam hao walifanya mawasilisho ya Mpango kazi kupitilia utekelezaji wa mradi, kama vile kazi za upembuzi yakinifu katika miradi ya kilimo cha umwagiliaji ambayo hufanyika kabla ya mradi kuanza na mradi kutekelezeka, jambo ambalo linapelekea ubora na uimara wa miundombinu ya umwagiliaji.
Sambamba na hilo, mawasilisho pia yalilenga katika majadiliano yaliyohusu tathmini na ufuatiliaji katika swala zima la matumizi na matunzo ya miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji hasa katika eneo la matunzo ya miundmbinu hiyo.
Mradi huo ulianza kazi kwa awamu ya kwanza kutoka December 2010 mpaka June 2014, awamu ya pili kutoka August 2015 mpaka August 2019 na kuongezewa muda kuanzia September 2019 mpaka August 2020 ambapo mradi huo unaofadhiliwa na Shirika na Kimataifa la maendeleo la Japan (JICA) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania utakwisha muda wake.
Comments
Post a Comment