Balozi Kingu naye aitikia wito wa TAKUKURU


Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Balozi Mteule, Meja Jenerali Jacob Kingu naye amefika katika ofisi za TAKUKURU jijini Dodoma ili kuhojiwa kufuatia agizo la Rais Dkt. John Magufuli kutokana na mkataba tata wa Tsh trilioni 1.04 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya zima moto.

Mwingine aliyewasili leo Ijumaa, Januari 31, 2020, kuhojiwa na TAKUKURU ni aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola ambaye amefika ofisini hapo mapema leo saa 1 asubuhi.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato