Posts

Showing posts from March, 2019

Mmoja afariki, watano wajeruhiwa katika mgogoro wa ardhi

Image
Mtu mmoja amefariki na wengine watano wamejeruhiwa  baada  ya  kushambuliwa kwa Mikuki, Mishale, Sime, Rungu na Fimbo katika vurugu za kugombea ardhi zilizotokea katika  kata  ya  Monduli juu  wilayani  Monduli  mkoani  Arusha. Picha: Majeruhi aliyelazwa katika hospitali ya wilaya ya Monduli, Lekishoy Mbasia mkazi wa kijiji Lendikinya wilayani Monduli akionyesha majeraha aliyoyapata mguuni Kwa kuchomwa na sime kufuatia baada ya kuibuka mgogoro wa kugombea mipaka kati ya vijiji viwili wilayani Monduli

Waziri wa Kilimo afungua Mkutano Mkuu wa TFA

Image
Waziri wa Kilimo Josephat Hasunga amefungua mkutano mkuu wa wanahisa wa shirikisho la Wakulima Tanganyika  (TFA) kilichowakutanisha wadau wa kilimo na wanahisa kwa pamoja ili kujadili maendeleo ya kilimo. Hasunga ameipongeza TFA kwa juhudi wanazozifanya katika kukuza sekta ya kilimo nchini ambayo ni kiinua mgongo na imeajiri watu wengi zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania. Akizungumza katika mkutano huo ambao uliambatana na utoaji wa vitambulisho vya kielektroniki kwa wakulima hao,amesema kuwa serikali itaendelea kushirikiana na TFA katika kutatua changamoto za wakulima ili kuboresha sekta ya kilimo. Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakulima TFA Peter Sirikwa amesema kuwa TFA iko mstari wa mbele katika kuhamasisha maendeleo ya kilimo nchini na kuwanganisha wadau wa kilimo kwa pamoja.

Watu 271 waambukizwa kipindupindu Msumbiji

Image
Idadi ya watu walioambukizwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Msumbiji imeongezeka mara dufu na kufikia 271,ikilinganaaishwa na idadi iliyotajwa siku moja kabla. Hayo yameelezwa na shirika la habari la Ureno, Lusa, likimnukuu mkurugenzi wa kitengo cha taifa cha afya nchini Msumbiji, Ussein Isse. Hadi sasa hakuna yeyote aliyeripotiwa kufariki kutokana na ugonjwa huo hatari.  Ugonjwa wa kipindupindu umegunduliwa katika mji wenye bandari wa Beira, ambako shirika la madaktari wasio na mpaka limesema kila siku linawaona watu wapatao 200 wenye dalili za ugonjwa huo. Katika ripoti nyingine, shirika la habari la Lusa limesema idadi ya watu waliofariki kufuatia kimbunga Idai nchini Msumbiji imefikia watu 501, huku maafisa wa nchi hiyo wakitoa tahadhari kwamba idadi ya vifo itazidi kuongezeka kadri miili ya wahanga wa mafuriko itakavyozidi kupatikana.

Naibu Waziri wa Madini ashtukia mchezo mchafu, wananchi waibiwa madini bila kujijua

Image
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amefunga mitambo yote ya kuchenjulia madini ya dhahabu Wilayani Kahama baada ya kubaini udanganyifu mkubwa kwenye uchenjuaji wa madini. Naibu Waziri Nyongo amechukua hatua hiyo kwenye ziara yake aliyoifanya jana Wilayani Kahama yenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini. Akiwa katika ziara hiyo, alifanya ziara ya kushtukiza katika kampuni ya kuchenjua madini ya dhahabu ya Ng’ana Group inayomilikiwa na  Theogenes Zacharia pamoja na mwenzake aliyejulikana kwa jina la Antidius na kubaini kampuni hiyo imekuwa ikiwaibia wateja wake kupitia mfumo wa uchenjuaji wa madini ya dhahabu. Naibu Waziri alioneshwa na wataalam kutoka Wizara ya Madini na Tume ya Madini waliopewa kazi maalum ya kuchunguza mfumo wa uchenjuaji wa dhahabu wa kampuni hiyo, sehemu ya mabomba ya mfumo iliyoharibiwa kwa makusudi kwa lengo la kunasa kiasi cha dhahabu kabla ya kufikishwa katika chomb...

Ni noma: Simba SC washinda mechi 10 mfululizo Ligi Kuu

Image
Hapo jana timu ya Simba SC ilishinda mchezo wake wa 10 mfululizo kwenye Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL) mara baada ya kuwachapa Mbao FC goli 3-0. Kwa matokeo hayo Simba wanafikisha pointi 57 wakiwa wamecheza michezo 22, huku wakiendelea kusalia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi hiyo ambapo hadi Yanga wanaongoza. Kwa mchezo wa jana John Bocco ndiye alianza kufunga bao la kuongoza kwa Simba dakika ya 24 akimalizia faulo iliyopigwa na Mohamed Hussein. Bocco alipachika bao la pili mkwaju wa penalti baada ya mchezaji wa Mbao FC, Peter Mwangosi kunawa mpira uliopigwa na Mzamiru Yassin dakika ya 58, huku Meddie Kagere alipachika bao la tatu  baada ya beki  wa Mbao kumchezea rafu Kagere eneo la hatari na mwamuzi kutoa penalti iliyopigwa na Kagere dakika ya 79 ya mchezo huo.

Dudu Baya aiomba radhi familia ya Ruge Mutahaba

Image
Msanii wa Bongo Fleva, Dudu Baya ameiomba radhi jamii na familia ya Marehemu Ruge Mutahaba kutokana na maneno yake ya dhihaka aliyowahi kuyatoa kipindi cha msiba. Pia msanii huyo ameliomba radhi Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kutokana na kuwahi kutoa matamshi yasiofaa kwa baraza hilo kipindi cha nyuma. Dudu Baya ametumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kwa kuweka video yake ya kuimba radhi na kuonyesha kujutia makosa yake. Utakumbuka mwishoni mwa February mwaka huu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe aliliagiza Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kushirikiana na Polisi kuhakikisha wanamkamata Msanii Dudu Baya kwa kosa la kukashifu na kutoa lugha za kejeli kwa Marehemu Ruge Mutahaba.

Tanzania yakamata nafasi 10 nchi zenye amani Afika

Image
Taswira ya Tanzania kimataifa imeendelea kupaa baada ya Taasisi ya Global Peace Index (GPI) kuitangaza Tanzania kushika nafasi ya 51 miongoni mwa nchi zenye amani zaidi duniani katika kipindi cha mwaka 2018. Tanzania imeshika nafasi hiyo ikiwa ni ya juu zaidi kufikiwa tangu mwaka 2010 na kuzishinda nchi kubwa duniani kama Marekani, China, Uingereza na Ajentina ambapo kwa Afrika ipo katika nafasi 10 bora na kuwa kinara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tangu Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli iingine madarakani, Tanzania imekuwa ikipanda nafasi kila mwaka ambapo mwaka 2017 ilishika nafasi ya 54, mwaka 2016 nafasi ya 58 na mwaka 2015 nafasi ya 64. Kwa miujibu wa GPI, sababu zilizoipaisha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye amani zaidi duniani ni pamoja na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika kupambana na rushwa, mgawanyo sahihi wa rasilimali, upatikanaji huru wa taarifa, mazingira wezeshi ya biashara, uhusiano ...

MAGAZETI YA LEO 1/4/2019

Image

VIDEO: Kocha wa Mbao akubali yaishe kwa Simba/ Alia na penati, warudi nyumbani kujipanga upya

Image
Kocha wa Mbao FC amekubali matokeo ya kufungwa mabao 3-0 na Simba katika mchezo wa ligi kuu uliochezwa katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro. Hata hivyo kocha huyo ameonyesha kuumizwa na penati mbili ambazo Simba walizipata lakini amesema kuwa anarudi nyumbani kwa ajili ya kujipanga upya. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAU KUSUBSCRIBE

Kanuni muhimu za kuishi maisha marefu katika ndoa

Image
Ndoa ni baraka hivyo ukipata shukuru, huu ni usemi ambao uliwahi kuibwa na msanii fulani hapa tanzania. Hakika nami naungana hoja yake pasipo kupinga kweli ndoa ni baraka kutoka Mwenyezi Mungu, hivyo unatakiwa kujua kanuni zitakazokusaidia kuishi maisha marefu katika ndoa yenu mpaka pale kifo kitakapowatenganisha. Zifuatazo ndizo kanuni muhimu za kuishi maisha marefu katika ndoa; Uhalisia wa maisha Jambo la msingi ambalo unatakiwa kuelewa ili kuweza kuishi maisha marefu na yenye baraka katika ndoa basi hutakiwi kuishi maisha ya kuigiza tena, bali unatakiwa kuishi yenye uhalisia, uwongo hauna nafasi tena, kwani ukisema bado unaishi kwa kumdabganya mwenza wako basi jua fika mahusoano yako hayatadumu. Hivyo kila wakati acha mara moja uwongo usikuwa na msaada wowote katika maisha yako katika ndoa. Upendo wa dhati. Kila mmoja wetu anahitaji kupendwa katika ulimwengu wa kimahusiano, hivyo kila wakati hakikisha unajitoa kwa dhati kumpenda yule umpendaye. Upendo wa dhati ndiyo utaku...

VIDEO: Aussems atema cheche/ Baada ya Mbao, JKT Tanzania watahadharishwa

Image
Kocha wa Simba Patrick Aussems, amefunguka baada ya kuifunga Mbao FC mabao 3-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara. Mchezo huo umeonekana ni kama wa kulipa kisasi baada ya Simba kufungwa bao 1-0 na timu hiyo kwenye mzunguko wa kwanza. Aussems pia amegusia mchezo wa na JKT Tanzania Jumatano ya April 3, 2019. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAU KUSUBSCRIBE

VIDEO: Tazama Penati ya Bocco na Kagere zilivyotaka kumtegua kipa wa Mbao

Image
Klabu ya soka ya Simba Jumapili hii imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mbao kwenye mchezo wa ligi kuu ambao umechezwa katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro. Katika mchezo huo Simba ilipata penati mbili. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAU KUSUBSCRIBE

Pacha wa Mo Dewji atikisa mechi ya Simba/ Afunguka kuhusu timu yake

Image
Mtu mmoja ambaye amefanana sana na bosi wa Sima, Mohammed Dewji, amewashtua mashabiki katikauwanja wa Jamuhuri Morogoro wakati wa mcezo wa ligi kuu kati ya Simba na Mbao. Pia mtu huyo amefunguka kuhusu mapenzi yake kwa timu ya Simba. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAU KUSUBSCRIBE