Kanuni muhimu za kuishi maisha marefu katika ndoa

Ndoa ni baraka hivyo ukipata shukuru, huu ni usemi ambao uliwahi kuibwa na msanii fulani hapa tanzania. Hakika nami naungana hoja yake pasipo kupinga kweli ndoa ni baraka kutoka Mwenyezi Mungu, hivyo unatakiwa kujua kanuni zitakazokusaidia kuishi maisha marefu katika ndoa yenu mpaka pale kifo kitakapowatenganisha.

Zifuatazo ndizo kanuni muhimu za kuishi maisha marefu katika ndoa;

Uhalisia wa maisha
Jambo la msingi ambalo unatakiwa kuelewa ili kuweza kuishi maisha marefu na yenye baraka katika ndoa basi hutakiwi kuishi maisha ya kuigiza tena, bali unatakiwa kuishi yenye uhalisia, uwongo hauna nafasi tena, kwani ukisema bado unaishi kwa kumdabganya mwenza wako basi jua fika mahusoano yako hayatadumu.

Hivyo kila wakati acha mara moja uwongo usikuwa na msaada wowote katika maisha yako katika ndoa.

Upendo wa dhati.
Kila mmoja wetu anahitaji kupendwa katika ulimwengu wa kimahusiano, hivyo kila wakati hakikisha unajitoa kwa dhati kumpenda yule umpendaye. Upendo wa dhati ndiyo utakufanya uweze kudumu katika mahusiano yako ya ndoa.

Utii kwa jamii yako.
Utii ndiyo silaha ya kudumu katika maisha ya mahusiano hivyo kila wakati unatakiwa kuelewa ili uweze katika maisha ya ndoa basi unatakiwa kumtii mwenza wako na jamii yako inayokuzunguka. Hakuna kitu kitakachokuwa na thamani kwako kama utaaamua kumtii  mwenza wako na jamii yako kwa ujumla.

Uvumilivu.
Msingi mkubwa wa neno ndoa ni uvumilivu, kwa hali ambayo mnaipitia katika maisha ya mahusiano husasani suala la kiuchumi basi unatakiwa kuwa mvumilivu, maisha yana kupanda na kushuka, hivyo pale mnapoyumba kiuchumi hutawi kuwa chachu au kigezo cha kuyasambalatisha mahusiano yenu bali unatakiwa kuwa mvumilivu tu kwani maisha  ndoa na uvumilivu hujenga mahusiano yalishibana.

Uaminifu.
Uli uweze kudumu katika maisha ya ndoa neno uaminifu linatakiwa kutawala maisha yenu kwa sehemu kubwa sana, kila wakati ukumbuke ule usemi mtamu usemao  michepuko siyo dili bali unatakiwa kubaki njia kuu.


Uwajibikaji katika kazi
Hakuna mtu ambaye anapenda mtu mvuvi katika maisha ya ndoa, hivyo kila wakati unatakiwa kuweza nguvu, akili, muda katika kufanya kazi, wajibika ipasavyo ili uweze kudumu katika maisha yako  ya ndoa. Fanya kazi kadri uwezavyo hata mwenzi wako atafurahia kuwa na wewe kila wakati.

Mwisho afisa mipango naomba niweke nukta kwa kusema Mwenyezi Mungu ndiye anayetakiwa kuyaongoza maisha yako ya ndoa kila wakati, muombe yeye ili aweze kuyaongoza kila wakati maisha yako ya ndoa, maana shetani siyo mtu mzuri maana wengine kila wanapojaribu kujenga mahusiano yao shetani anaiba cement, hivyo mtanguze Mungu kila wakati ili shetani asiyavuruge mahusiano yenu.

Na. Benson Chonya.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato