Dudu Baya aiomba radhi familia ya Ruge Mutahaba
Msanii wa Bongo Fleva, Dudu Baya ameiomba radhi jamii na familia ya Marehemu Ruge Mutahaba kutokana na maneno yake ya dhihaka aliyowahi kuyatoa kipindi cha msiba.
Pia msanii huyo ameliomba radhi Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kutokana na kuwahi kutoa matamshi yasiofaa kwa baraza hilo kipindi cha nyuma.
Dudu Baya ametumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kwa kuweka video yake ya kuimba radhi na kuonyesha kujutia makosa yake.
Utakumbuka mwishoni mwa February mwaka huu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe aliliagiza Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kushirikiana na Polisi kuhakikisha wanamkamata Msanii Dudu Baya kwa kosa la kukashifu na kutoa lugha za kejeli kwa Marehemu Ruge Mutahaba.
Comments
Post a Comment