Waziri wa Kilimo afungua Mkutano Mkuu wa TFA
Waziri wa Kilimo Josephat Hasunga amefungua mkutano mkuu wa wanahisa wa shirikisho la Wakulima Tanganyika (TFA) kilichowakutanisha wadau wa kilimo na wanahisa kwa pamoja ili kujadili maendeleo ya kilimo.
Hasunga ameipongeza TFA kwa juhudi wanazozifanya katika kukuza sekta ya kilimo nchini ambayo ni kiinua mgongo na imeajiri watu wengi zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania.
Akizungumza katika mkutano huo ambao uliambatana na utoaji wa vitambulisho vya kielektroniki kwa wakulima hao,amesema kuwa serikali itaendelea kushirikiana na TFA katika kutatua changamoto za wakulima ili kuboresha sekta ya kilimo.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakulima TFA Peter Sirikwa amesema kuwa TFA iko mstari wa mbele katika kuhamasisha maendeleo ya kilimo nchini na kuwanganisha wadau wa kilimo kwa pamoja.
Comments
Post a Comment