Watu 271 waambukizwa kipindupindu Msumbiji
Idadi ya watu walioambukizwa ugonjwa wa kipindupindu nchini Msumbiji imeongezeka mara dufu na kufikia 271,ikilinganaaishwa na idadi iliyotajwa siku moja kabla.
Hayo yameelezwa na shirika la habari la Ureno, Lusa, likimnukuu mkurugenzi wa kitengo cha taifa cha afya nchini Msumbiji, Ussein Isse. Hadi sasa hakuna yeyote aliyeripotiwa kufariki kutokana na ugonjwa huo hatari.
Ugonjwa wa kipindupindu umegunduliwa katika mji wenye bandari wa Beira, ambako shirika la madaktari wasio na mpaka limesema kila siku linawaona watu wapatao 200 wenye dalili za ugonjwa huo.
Katika ripoti nyingine, shirika la habari la Lusa limesema idadi ya watu waliofariki kufuatia kimbunga Idai nchini Msumbiji imefikia watu 501, huku maafisa wa nchi hiyo wakitoa tahadhari kwamba idadi ya vifo itazidi kuongezeka kadri miili ya wahanga wa mafuriko itakavyozidi kupatikana.
Comments
Post a Comment