Ni noma: Simba SC washinda mechi 10 mfululizo Ligi Kuu


Hapo jana timu ya Simba SC ilishinda mchezo wake wa 10 mfululizo kwenye Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL) mara baada ya kuwachapa Mbao FC goli 3-0.

Kwa matokeo hayo Simba wanafikisha pointi 57 wakiwa wamecheza michezo 22, huku wakiendelea kusalia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi hiyo ambapo hadi Yanga wanaongoza.

Kwa mchezo wa jana John Bocco ndiye alianza kufunga bao la kuongoza kwa Simba dakika ya 24 akimalizia faulo iliyopigwa na Mohamed Hussein. Bocco alipachika bao la pili mkwaju wa penalti baada ya mchezaji wa Mbao FC, Peter Mwangosi kunawa mpira uliopigwa na Mzamiru Yassin dakika ya 58, huku Meddie Kagere alipachika bao la tatu  baada ya beki  wa Mbao kumchezea rafu Kagere eneo la hatari na mwamuzi kutoa penalti iliyopigwa na Kagere dakika ya 79 ya mchezo huo.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato