Posts

Showing posts from July, 2020

MAGAZETI YA LEO 1/8/2020

Image

Wakosoaji wapinga uamuzi wa kuahirisha uchaguzi Hong Kong

Image
Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam leo ameahirisha uchaguzi wa bunge wa Septemba 6 kwa mwaka moja, kwa sababu ya kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona. Hatua hiyo ni pigo kwa wapinzani wanaopigania demokrasi Hong Kong, ambao walitaumaini kushinda wingi wa viti bungeni. Uamuzi huo umetangazwa baada ya wagombea 12 wa upande wa upinzani kuzuwiwa kugombea katika uchaguzi huo kwa madai ya uchochezi, pamoja na kuipinga sheria mpya ya usalama wa kitaifa iliyotangazwa na China. Hatua hiyo imezua shaka iwapo janga la corona ndiyo sababu ya kweli ya kusogezwa mbele uchaguzi. Lam amesema uamuzi wake huo haukuchochewa na maslahi ya kisiasa.

Picha zamfikisha tena Nandy BASATA

Image
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza  amesema sababu ya kumwita msanii Nandy ofisini kwao jana Julao 30, ni kutokana na picha alizopost kwenye mtandao wa Instagram ambapo kwa mujibu wa Basata wamesema sio picha nzuri. Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Godfrey Mngereza amesema kuwa wamemwita kuzungumzia kuhusu utaratibu wa picha alizopost Instagram ambazo hazikuwa nzuri. "Mara nyingi tumekuwa na utaratibu wa kuzungumza na wasanii, kuna picha kadhaa ambazo alikuwa amezirusha kwenye mtandao wa Instagram yake ambazo hazikuwa nzuri, kwa hiyo mahali alipofikia yeye si vizuri kupost picha kama zile,  vilevile kuwa makini na suala la mitandao hivyo ndiyo vitu tulivyomkumbusha tena kwa njia chanya kabisa, sisi kama Basata tuna wajibu wa kuwakumbusha wasanii kabla hatujaenda kwenye upande wa adhabu" Katibu Mtendaji Basata Godfrey Mngereza

Mamia waandamana baada ya askari walevi kuua watu 13 DRC

Image
Askari waliokuwa wamelewa nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamemimina risasi na kuua watu 13 na wengine kadhaa kujeruhiwa. Mmoja wa wahanga anaripotiwa kuwa mtoto wa miaka miwili. Mauaji hayo yalitokea usiku wa Alhamisi katika jimbo la Kivu kusini mashariki mwa nchi hiyo Jeshi la Jamuhuri ya demokrasia ya Kongo linawatafuta askari hao waliouwa watu 13, wakiwemo wanawake na watoto katika mji wa Uvira. Makundi kadhaa ya wanajeshi pamoja na walinda amani wa Umoja wa mataifa wako katika mji huo ili kuwalinda raia. Ni siku ya masikitiko makubwa katika fukwe za ziwa Tanganyika, kumekuwa na waandamanaji wenye hasira dhidi jeshi la Kongo katika mji wa Sange, tangu majira ya asubuhi eneo ambalo barabara nyingi zilikuwa zimefugwa. Waandamanaji hao wanataka familia zilizoathirika kulipwa fidia na huduma za afya kwa wale waliojeruhiwa. Jeshi limeiambia BBC kuwa askari wale walifanya tukio hilo kwa sababu walikuwa wamelewa na watafukuzwa jeshini na kuchukuliwa hatua za kishe...

Serikali ya Afghanistan yawaachia wafungwa zaidi wa Taliban

Image
Mpango wa siku tatu wa kusitisha mapigano umeanza kutekelezwa nchini Afghanstan, wakati waumini wa dini ya Kiislamu wakisherehekea sikukuu ya Eid al-Adha. Kuna matumaini kwamba mapatano hayo ya muda na ubadilishanaji wafungwa vitapelekea kufanyika mazungumzo ya amani kati ya kundi la Taliban na serikali ya Afghanistan. Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani aliamuru kuachiliwa huru kwa wafungwa wengine 50 wa Taliban mapema leo, wakati mpango huo wa usitishaji mapigano kwa masaa 72 ukianza. Mapatano hayo yaliopendekezwa na Taliban na kukubaliwa na serikali mjini Kabul, yanatarajiwa kudumu kwa kipindi cha siku tatu za sherehe ya Eid al-Adha, na hatimaye kusafisha njia ya kufanyika kwa mazungumzo ya amani yaliosubiriwa kwa muda mrefu kati ya pande hizo mbili zinazohasimiana. Kusitishwa kwa mapigano na kubadilishana wafungwa - kulikojadiliwa katika makubaliano kati ya Taliban na Marekani mnamo mwezi Februari - ndiyo masharti ya kuanza kwa mazungumzo kati ya wa Afghanistan.

Meneja wa Harmonize afunguka kumng'oa msanii huyo

Image
Meneja wa msanii Harmonize Dr Sebastian Ndege maarufu kama Jembe ni Jembe, amesema alikuwa anatuhumiwa na watu suala la kumchukua Harmonize kwenye menejimenti aliyokuwa ili aweze kufanya naye biashara. Akizungumza kwenye Show ya SalamaNa inayoruka kila siku ya Alhamisi saa 3:00 usiku kupitia East Africa TV, Sebastian Ndege amesema kuna hisia tatu ambazo watu walikuwa na mashaka naye wakati anamchukua Harmonize. "Kuna hisia tatu ambazo watu walikuwa wana mashaka mimi kuwa meneja wa Harmonize, moja ni kumfelisha dogo, mbili ni kumpoteza tatu ni kumtoa WCB, lakini ukweli ni kwamba mimi nilisubiri muda wake uishe ili niweze kufanya naye kazi" amesema Meneja wa Harmonize Dr Sebastian Ndege 

Maandamano ya upinzani Belarus yavutia watu 34,000

Image
Hapo jana, maelfu ya watu wameshiriki katika maandamano ya upinzani katika mji mkuu wa Belarus, Minsk, ikiwa ni takriban wiki moja kabla ya uchaguzi wa rais nchini humo. Shirika ka kutetea haki za binadamu Viasna, limesema mwanasiasa Svetlana Tikhanovskaya aliyeitisha maandamano hayo, ameitikiwa na watu wapatao elfu thelathini na nne. Ni maandamano makubwa zaidi ya upinzani kuwahi kushuhudiwa katika jamhuri hiyo ya zamani ya Kisovieti. Katika uchaguzi huo ujao, Tikhanovskaya anatarajiwa kuchuana na Rais Alexander Lukashenko aliye madarakani kwa miaka 26, na ambaye anawania muhula wake wa sita madarakani. Wasimamizi wa kimataifa mara kwa mara wamekuwa wakikosoa chaguzi za Belarus, wakisema huwa zinashindwa kufuata kanuni za demokrasia.

Uchumi wa Ufaransa umeanguka kutokana na corona

Image
Kama ilivyo nchini Ujerumani na Marekani, Ufaransa nayo imetangaza kuporomoka kwa uchumi wake kutokana na janga la virusi vya corona. Katika robo ya pili ya mwaka, uchumi wa Ufaransa umenywea kwa asilimia 13.8 kulingana na ofisi ya takwimu ya mjini Paris. Tangu robo ya kwanza ya mwaka, kulionekana dalili za athari za janga la corona katika uchumi wa Ufaransa ambao ni wa pili kwa ukubwa katika kanda inayotumia sarafu ya euro. Hapo jana, Ujerumani imetangaza kuporomoka kwa uchumi wake kwa asilimia 10, na Marekani imeshuhudia kuanguka kwa uchumi wake kwa thuluthi moja.

Marekani yatoa ilani ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran

Image
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema nchi yake italazimisha vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran ikiwa muda wa vikwazo vya silaha vya hapo awali utamalizika. Urusi na China zenye kura ya turufu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zinataka Iran iuziwe silaha za kawaida baada ya muda wa vikwazo hivyo kumalizika mwezi Oktoba. Vikwazo hiyvo viliwekwa kwa mujibu wa azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka wa 2015. Waziri Pompeo ameiambia kamati ya mambo ya nje ya baraza la seneti la Marekani kwamba nchi hiyo itapendekeza azimio la kurefusha muda wa vikwazo hivyo vya sasa. Waziri huyo ametamka kwamba ikiwa azimio hilo halitapitishwa, Marekani itachukua hatua za lazima kuhakikisha kwamba Iran inaendelea kuwekewa vikwazo. Hata hivyo wanachama wengine wa kudumu kwenye Baraza la Usalama Uingereza na Ufaransa wamesema suala la kipaumbele ni kutafuta suluhisho la kidiplomasia ili kukomesha mpango wa nyuklia wa Iran, ingawa pia zinaunga mkono vikwazo dhidi ya Ira...

Masoko ya hisa duniani yaporomoka

Image
Masoko ya hisa duniani na masoko ya hisa nchini Marekani yamelegalega baada ya hazina ya Marekani kuonya kwamba janga la virusi vya corona huenda likatishia uchumi uliorejea katika hali ya kawaida uliyoweka viwango vya riba karibu ya sifuri. Kuanguka kwa hisa kuliongezeka kwa kasi katika mataifa ya Ulaya baada ya Ujerumani kusema uchumi wake ulinywea kwa asilimia 10 katika robo ya pili kwenye kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Viwango vya chini vya riba na matarajio ya wawekezaji juu ya uwezekano wa kupatikana kwa chanjo dhidi ya virusi vya corona vilisaidia masoko ya dunia kuwa kwenye hali nzuri katika sehemu kubwa ya mwaka huu.

Ujerumani yasema Marekeni haipaswi kuzuia uteuzi wa mjumbe mpya wa Libya.

Image
Balozi wa Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa amesema Marekani haipaswi kumzuia katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kumteua mjumbe mpya wa kuushughulikia mgogoro wa nchini Libya. Balozi Christoph Heusgen ametoa tahadhari hiyo kutokana na taarifaa kwamba Marekani inataka wadhifa huo ugawanywe katika sehemu mbili. Marekani inataka kuwepo mjumbe atakayesimamia masuala ya kisiasa na ya kuleta amani nchini Libya na mjumbe mwengine atakayesimamia juhudi za kuleta usuluhishi. Hata hivyo baadhi ya wanachama wa Baraza la Usalama hawakubaliani na pendekezo hilo la Marekani. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa wa hapo awali Ghassan Salame alijiuzulu miezi mitano iliyopita kutokana na uchovu baada ya juhudi zake kushindikana. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amempendekeza aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Ghana Hanna Tetteh ambaye kwa sasa ni mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika Umoja wa Afrika.

China na Urusi zawekewa vikwazo na Umoja wa Ulaya

Image
Umoja wa Ulaya umeziwekea China, Urusi na Korea Kaskazini vikwazo kwa kuwapiga marufuku maafisa wa idara za ujasusi za nchi hizo kuingia katika nchi za Umoja wa Ulaya. Umoja wa Ulaya umechukua hatua hiyo kutokana na idara hizo kutuhumiwa kushiriki katika shughuli za udukuzi wa kimtandao duniani kote. Idara hizo za ujasusi zinatuhumiwa kujaribu kufanya udukuzi kwenye shirika la kudhibiti silaha za nyuklia. Waliowekewa vikwazo hiyvo ni maafisa sita na taasisi kadhaa za nchi hizo tatu. Na kwa ajili ya kujihami dhidi ya hujuma za kimtandao Umoja wa Ulaya ulipitisha utaratibu wa kisheria wa kuuwezesha kuweka vikwazo. Vikwazo vya Umoja wa Ulaya pia vitahusu kuzuia mali za watu na hata za taasisi.

EDD MUBARAK

Image
Uongozi wa Muungwana Blog pamoja na wafanyakazi wake wote tunapenda kuwatakia heri ya sikukuu ya Eid Hajj Waislamu wote nchini. Muungwana Blog inawatakia sikukuu njema! Eid Mubarak, Pia msisahau kujikinga na Corona.

Takukuru Manyara wamnasa Alute kwa kufanya biashara ya Mikopo Kitapeli akitumia jina la Halmashauri

Image
Na John Walter-Babati Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa  (TAKUKURU) mkoa wa Manyara inamshikilia mfanyabiashara Japhet Samwel Alute kwa kukwepa kulipa kodi ya serikali na kufanya biashara bila kuwa na leseni. Mkuu wa Takukuru mkoani hapa Holle Makungu amesema kuwa mtu huyo pia anatoa mikopo umiza kwa wananchi kwa riba kubwa na kisha kuwadhulumu mali zao wanazoweka kama dhamana. Makungu amesema kuwa Alute pia anawatishia wananchi wanaochelewa kufanya marejesho  kwa kutumia jina  la Halmashauri ya Mji wa Babati kwa kuwatumia ujumbe wa kuwauzia maeneo yao au nyumba walizoweka kama dhamana kwa mikopo umiza. Amesema katika upekuzi walioufanya kwa mfanyabiashara huyo  wamekuta  mikataba ya kitapeli 99 ambayo inaonyesha ameuziwa maeneo mbalimbali zikiwemo nyumba na viwanja vya baadhi ya wananchi wa Mji wa Babati. Aidha mtuhumiwa amekutwa akiwa na vitambulisho vya watumishi wa Umma na uraia wa Tanzania ambavyo si Mali yake. Mkuu huyo  wa TAKUKUR...

Ushuhuda wa wanawake waliotekwa, kubakwa na kugombolewa DRC

Image
Wanawake nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameliambia shirika la waangalizi wa haki za binaadamu madhila waliyoyapitia ya kutekwa nyara kwa ajili ya kupata fedha. vitendo vilivyotekelezwa na magenge ya wahalifu Wengi wa walioshikiliwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita walitekwa wakiwa mashambani walikokuwa wakifanya kazi zao, kisha wakashurutishwa kutembea saa kadhaa kuelekea hifadhi ya taifa ya Virunga, eneo la urithi la shirika la Umoja wa Mataifa la sayansi na utamaduni UNESCO, ambako walikuwa wakishikiliwa na kupigwa. Kisha waliwasiliana na familia za wanaowashikilia na kuwataka kutoa fedha ili wawaachilie. ''Walituonesha mifupa ya binadamu na kusema kuwa ni watu waliowaua baada ya kukiuka amri zao,'' alisema manusura Yolande. ''Kuna nyakati walizima simu zao ili kuongeza shinikizo kwa familia hizo kwa kuwa hawakufurahia ofa zilizokuwa zikitolewa. Mateka wa kiume walipigwa vibaya zaidi.'' Wanawake na wasichana walikuwa wak...
Image
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma ACP James Manyama, amesema kuwa watu 10 wamefariki Dunia huku wengine 100  wakiokolewa, baada ya Boti iliyokuwa ikitokea maeneo ya Sibosa kupigwa na dhoruba kisha kugonga mwamba na kupasuka ndani ya Ziwa Tanganyika. Kamanda Manyama ametoa taarifa hiyo hii leo Julai 31, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, ambapo amesema kuwa ajali hiyo ilitokea jana Julai 30 majira ya saa 5:00 Asubuhi. "Boti iloikuwa na watu karibia 100, na ilipokuwa ndani ya maji ilikumbwa na dhoruba kali na kugonga mwamba kisha kupasuka, na watu takribani 100 wameokolewa na kusababisha vifo vya watu 10, Wanawake3, Mwanaume 1 na watoto 6, zoezi la uokoaji linaendelea leo tuna mashaka huenda kuna miili ndani ya maji" amesema Kamanda Manyama. Aidha kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Uvinza  Dkt Ruben Mwakilima, amesema kuwa miili imehifadhiwa katika Zahanati ya kalya na tayari miili ya watu wanne imekwishachukuliwa na ndugu zao

Sheikh Mkuu Dar awaasa wagombea kufanya kampeni za utu na heshima

Image
Wanasiasa wameaswa kufanya kampeni za utu na heshima ili kuendelea kulinda amani iliyopo nchini. Hayo yamezungumzwa na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salim katika viwanja vya mnazi mmoja iliposwaliwa swala ya Eid. Mbali na hilo Sheikh Alhad amesema dini ya uislam inafundisha amani, mshikamano na ushirikiano hivyo ni vema kupeana kushirikiana kwa ustawi wa amani na maendeleo nchini.

Tshishimbi afunguka kuhusu hatima yake ndani ya Yanga

Image
NAHODHA wa Yanga, Papy Tshishimbi amesema kuwa kuhusu kubaki ndani ya Yanga msimu ujao anamwachia Mungu. Mkataba wa Yanga na Papy Tshishimbi unafika tamati mwezi Agosti ambao kwa sasa umebakiza siku moja kwa kuwa leo ni Julai 31, kesho ni Agosti Mosi kabla ya nyota huyo kufikia siku yake aliyosaini kuwa mchezaji huru. Kumekuwa na mvutano mkubwa wa nyota huyo na Yanga kuhusu suala lake la kuongeza kandarasi mpya hali ambayo imemfanya nyota huyo kutomwaga saini mpaka sasa licha ya kupewa mkataba. "Suala la mimi kubaki ndani ya Yanga kwa msimu ujao ninamuachia Mungu kwani nimekuwa nikiskia habari nyingi ambazo zinanizungumzia mimi lakini hazina ukweli. "Naona viongozi wameanza kufanya mambo ambayo sio mazuri kwa kuzungumza kwamba wamenipa mkataba na kunipa siku za kusaini jambo ambalo sio sawa unapozungumzia mkataba sio jambo la kuzungumza kwenye vyombo vya habari. "Kwa sasa sina furaha ndani ya Yanga kwa kuwa hakuna ambacho tumeweza kufanikiwa hakuna taji tulilo...

Tetesi za soka za kimataifa

Image
Uhamisho unaokisiwa wa Jadon Sancho kwenda Manchester United uko karibuni kufikiwa, wakati Borussia Dortmund wakiwa tayari kukubali ada ya awali ya pauni milioni 60 kwa ajili ya winga huyo, 20. (Independent) Mshambuliaji wa Mexico Raul Jimenez, 29, yuko njiani kuelekea Manchester United baada ya Wolves kukubali ada ya pauni milioni 27 kumsajili mshambuliaji wa Braga, Mreno Paulinho. (RTP,Express) Gareth Bale, 31, amemwambia kocha wa Wales Ryan Giggs kuwa ana dhamira ya kusalia Real Madrid msimu ujao. hata kama kukosa michezo kutaathiri kipato chake. (Mirror) Chelsea na Manchester City ni miongoni mwa vilabu vinavyoongoza ambavyo vinafuatilia kama mchezaji David Alaba, 28, atasaini mkataba mpya na Bayern Munich. (Telegraph) Leeds wanapanga kusajili wachezaji wawili- Kiungo wa Everton Fabian Delph, 30, na beki Danny Rose,30, wakati huu ambapo kocha Marcelo Bielsa akitafuta wachezaji wenye uzoefu na ligi ya primia. (Star) Mlinda mlango Muajentina Sergio Romero,33, anataka kufan...

Tekashi 69 kuachiwa huru rasmi wikiendi hii

Image
Rapa machachari asiyeishiwa vituko kutoka pande za Brooklyn Marekani, Tekashi 69 anatarajia kuwa mtu huru kabisa, ambapo Leo Julai 30, anakua kabakiza siku tatu pekee kumalizia kifungo chake cha nje ambacho amekua akitumikia nyumbani kwake kwa muda wa miezi minne iliyopita. Itakumbukwa, kwa karibu miaka miwili sasa rapa huyo amekua kifungoni kutokana na hukumu aliyoipata baada ya kupatikana na hatia ya makosa tisa ikiwemo kufanya malipo na umiliki wa silaha za moto makosa ambayo yangemfanya #Tekashi atumikie miaka 32 nyuma ya nondo, lakini Disemba 18, 2019, #Tekashi alipunguziwa hukumu na kufikia miezi 24 baada ya kutoa ushirikiano kwa serikali. Muwakilishi kutoka upande wa 6ix9ine amethibitisha kuwa rapa huyo anatarajiwa kuachiliwa rasmi Jumapili hii Agosti 2. Sanjali na hilo, mtandao wa Page Six umeripoti kuwa, kwasasa #Tekashi ataimarisha ulinzi wake zaidi pindi atakapokuwa huru uraiani.

Picha: Rais Magufuli alivyoshuka na kutembea daraja la Mkapa

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipita na kukagua Daraja la Mkapa linalopita katika Mto Rufiji mkoani Pwani wakati akitokea Masasi Mtwara kwenye msiba wa Marehemu Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa leo tarehe 30 Julai 2020. Daraja hilo linalounganisha Pwani na Mikoa ya Lindi na Mtwara  lina urefu wa mita 970 na lilijengwa na Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Marehemu Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa. Lilifunguliwa Agosti 2, 2003

Waziri Hasuna atoa siku 14 kwa mkurugenzi wa bodi ya nafaka kukamilisha malipo ya wakulima wa korosho

Image
Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akiongozana na Meneja wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Kanda ya Arusha Ndg Idd Mkomalasa wakati alipotembelea CPB kukagua bidhaa zinazozalishwa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko wakati alipotembelea na kukagua ufanisi wa kinu cha kukoboa nafaka wakati akiwa katika ziara ya kikazi Jijini Arusha hivi karibuni. Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga ametoa siku 14 kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko Dkt Anslem Moshi kukamilisha malipo ya wakulima wote waliouza korosho msimu wa mwaka 2018/2019. Waziri Hasunga ametoa agizo hilo wakati alipotembelea na kukagua shughuli za utendaji kazi zinazofanywa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Jijini Arusha. Amesema kuwa Bodi hiyo ilipewa dhamana la kununua korosho mwaka 2018 kwa niaba ya serikali na tayari serikali imeshatoa fedha zote kwa ajili ya wakulima lakini bado CPB haijakamilisha malipo hivyo ni lazima malipo yakamilike ndani ya...

Kubadirisha wanaume ni kujitia aibu- Nuh Mziwanda

Image
Msanii wa muziki nchini, Nuh Mziwanda amemueleza aliyekuwa mpenzi wake Shilole, endapo ataachana na Uchebe atakuwa anajitia aibu. Kauli ya Nuh inakuja mara baada ya hivi karibuni Shilole kuibuka na kueleza kuwa amekuwa akiambulia vipigo katika ndoa yake ambayo kwa sasa ina mitikisiko. “Shilole kashakuwa mtu mzima aangalie cha kufanya maana kubadili wanaume ni kujitia aibu kila mtu ana mapungufu, aka echini na mumewe wayaongee yaishe,” amesema Nuh kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni. Itakumbukwa kuwa, Shilole na Nuh Mziwanda kipindi cha nyuma walikuwa wapenzi. Baada ya kuachana kwao, Nuh alienda kumuoa mrembo aitwaye #Nawal lakini baada ya kupata mtoto wao wa kwanza ndoa yao ilivunjika, baada ya muda Shilole aliolewa na #Uchebe.

MAGAZETI YA LEO 31/7/2020

Image