Kubadirisha wanaume ni kujitia aibu- Nuh Mziwanda

Msanii wa muziki nchini, Nuh Mziwanda amemueleza aliyekuwa mpenzi wake Shilole, endapo ataachana na Uchebe atakuwa anajitia aibu.

Kauli ya Nuh inakuja mara baada ya hivi karibuni Shilole kuibuka na kueleza kuwa amekuwa akiambulia vipigo katika ndoa yake ambayo kwa sasa ina mitikisiko.

“Shilole kashakuwa mtu mzima aangalie cha kufanya maana kubadili wanaume ni kujitia aibu kila mtu ana mapungufu, aka echini na mumewe wayaongee yaishe,” amesema Nuh kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni.

Itakumbukwa kuwa, Shilole na Nuh Mziwanda kipindi cha nyuma walikuwa wapenzi. Baada ya kuachana kwao, Nuh alienda kumuoa mrembo aitwaye #Nawal lakini baada ya kupata mtoto wao wa kwanza ndoa yao ilivunjika, baada ya muda Shilole aliolewa na #Uchebe.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato