Ujerumani yasema Marekeni haipaswi kuzuia uteuzi wa mjumbe mpya wa Libya.
Balozi wa Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa amesema Marekani haipaswi kumzuia katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kumteua mjumbe mpya wa kuushughulikia mgogoro wa nchini Libya. Balozi Christoph Heusgen ametoa tahadhari hiyo kutokana na taarifaa kwamba Marekani inataka wadhifa huo ugawanywe katika sehemu mbili.
Marekani inataka kuwepo mjumbe atakayesimamia masuala ya kisiasa na ya kuleta amani nchini Libya na mjumbe mwengine atakayesimamia juhudi za kuleta usuluhishi.
Hata hivyo baadhi ya wanachama wa Baraza la Usalama hawakubaliani na pendekezo hilo la Marekani. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa wa hapo awali Ghassan Salame alijiuzulu miezi mitano iliyopita kutokana na uchovu baada ya juhudi zake kushindikana.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amempendekeza aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Ghana Hanna Tetteh ambaye kwa sasa ni mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika Umoja wa Afrika.

Comments
Post a Comment