Maandamano ya upinzani Belarus yavutia watu 34,000
Hapo jana, maelfu ya watu wameshiriki katika maandamano ya upinzani katika mji mkuu wa Belarus, Minsk, ikiwa ni takriban wiki moja kabla ya uchaguzi wa rais nchini humo. Shirika ka kutetea haki za binadamu Viasna, limesema mwanasiasa Svetlana Tikhanovskaya aliyeitisha maandamano hayo, ameitikiwa na watu wapatao elfu thelathini na nne.
Ni maandamano makubwa zaidi ya upinzani kuwahi kushuhudiwa katika jamhuri hiyo ya zamani ya Kisovieti. Katika uchaguzi huo ujao, Tikhanovskaya anatarajiwa kuchuana na Rais Alexander Lukashenko aliye madarakani kwa miaka 26, na ambaye anawania muhula wake wa sita madarakani.
Wasimamizi wa kimataifa mara kwa mara wamekuwa wakikosoa chaguzi za Belarus, wakisema huwa zinashindwa kufuata kanuni za demokrasia.

Comments
Post a Comment