Wakosoaji wapinga uamuzi wa kuahirisha uchaguzi Hong Kong
Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam leo ameahirisha uchaguzi wa bunge wa Septemba 6 kwa mwaka moja, kwa sababu ya kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona.
Hatua hiyo ni pigo kwa wapinzani wanaopigania demokrasi Hong Kong, ambao walitaumaini kushinda wingi wa viti bungeni.
Uamuzi huo umetangazwa baada ya wagombea 12 wa upande wa upinzani kuzuwiwa kugombea katika uchaguzi huo kwa madai ya uchochezi, pamoja na kuipinga sheria mpya ya usalama wa kitaifa iliyotangazwa na China.
Hatua hiyo imezua shaka iwapo janga la corona ndiyo sababu ya kweli ya kusogezwa mbele uchaguzi. Lam amesema uamuzi wake huo haukuchochewa na maslahi ya kisiasa.

Comments
Post a Comment