Mwenyekitwa Halmashauri ya Iramba mkoani Singida, Simon Tyosela ameishauri serikali kuhalalisha biashara ya akina dada wanaoujiuza, maarufu machangudoa. Amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua ukusanyaji mapato ya halmashauri mbalimbali nchini. Alitoa ushauri huo, kutokana na kauli ya Mkuu wa Mkoa, Dk Rehema Nchimbi kueleza kuwa madada poa na machangudoa wote mjini hapo kukamatwa. Dk Nchimbi alitoa kauli hiyo wakati wa Kikao Maalumu cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichopitia na kupitisha Mpango wa Bajeti kwa Mwaka 2019/2020. Tyosela amesema kutokana na halmashauri nyingi nchini kukwama kukusanya mapato, ingekuwa jambo jema kama serikali ingehalalisha biashara ya machangudoa kama zilivyo biashara nyingine. "Niseme sikubaliani kamwe na suala la ushoga. Lakini hili la machangudoa nashauri lirasimishwe ili serikali iweze kujipatia mapato,"alisema na kuongeza "Iwapo watashindwa kulipa kodi hiyo, basi watakuwa wamejiondoa kwa hiyari yao wen...
Comments
Post a Comment