Uchumi wa Ufaransa umeanguka kutokana na corona

Kama ilivyo nchini Ujerumani na Marekani, Ufaransa nayo imetangaza kuporomoka kwa uchumi wake kutokana na janga la virusi vya corona.

Katika robo ya pili ya mwaka, uchumi wa Ufaransa umenywea kwa asilimia 13.8 kulingana na ofisi ya takwimu ya mjini Paris.

Tangu robo ya kwanza ya mwaka, kulionekana dalili za athari za janga la corona katika uchumi wa Ufaransa ambao ni wa pili kwa ukubwa katika kanda inayotumia sarafu ya euro.

Hapo jana, Ujerumani imetangaza kuporomoka kwa uchumi wake kwa asilimia 10, na Marekani imeshuhudia kuanguka kwa uchumi wake kwa thuluthi moja.


Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato