Takukuru Manyara wamnasa Alute kwa kufanya biashara ya Mikopo Kitapeli akitumia jina la Halmashauri

Na John Walter-Babati
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa  (TAKUKURU) mkoa wa Manyara inamshikilia mfanyabiashara Japhet Samwel Alute kwa kukwepa kulipa kodi ya serikali na kufanya biashara bila kuwa na leseni.

Mkuu wa Takukuru mkoani hapa Holle Makungu amesema kuwa mtu huyo pia anatoa mikopo umiza kwa wananchi kwa riba kubwa na kisha kuwadhulumu mali zao wanazoweka kama dhamana.

Makungu amesema kuwa Alute pia anawatishia wananchi wanaochelewa kufanya marejesho  kwa kutumia jina  la Halmashauri ya Mji wa Babati kwa kuwatumia ujumbe wa kuwauzia maeneo yao au nyumba walizoweka kama dhamana kwa mikopo umiza.

Amesema katika upekuzi walioufanya kwa mfanyabiashara huyo  wamekuta  mikataba ya kitapeli 99 ambayo inaonyesha ameuziwa maeneo mbalimbali zikiwemo nyumba na viwanja vya baadhi ya wananchi wa Mji wa Babati.

Aidha mtuhumiwa amekutwa akiwa na vitambulisho vya watumishi wa Umma na uraia wa Tanzania ambavyo si Mali yake.

Mkuu huyo  wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara Holle Makungu ametoa wito  kwa wote waliokumbana na mikopo hiyo umiza ya Alute au Mali zao kuchukuliwa kutokana na mikopo hiyo, wafike Ofisi za Takukuru Manyara Mtaa wa Miomboni mjini Babati siku ya Jumatatu Agosti 3,2020 ili Changamoto za mikopo umiza ziweze kupatiwa ufumbuzi.


Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato