Posts

Showing posts from January, 2019

Viwanja Vikubwa Vinauzwa: Bunju na Mapinga (Baobab sec)

Image
Viwanja viko Mingoi, ni mpakani mwa Bunju na Mapinga. Viko umbali wa km 2 kutoka Darajani (Bagamoyo Road). Viwanja viko sehemu nzuri inayofaa kwa Makazi, Biashara na Ufugaji. Viko Viwanja vya size tofauti: 20/20 (sqm 400) bei milion 5 20/30 (sqm 600) bei milion 8 20/40 (sqm 800) bei milion 10 Robo eka (32/32) bei milion 12 Nusu eka (32/64) bei milion 24 Eka nzima (64/64) bei milion 48 Luksa kulipa kwa awamu 2, kianzio ni 75% na luksa kujenga mara tu baada ya kulipa awamu ya kwanza. Biashara hii haina dalali/udalali. Mpigie Mhusika: call 0758603077, whatsap 0757489709 Ukipata ujumbe huu, mjulishe ndugu/jamaa/rafiki.

Rais Magufuli kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo

Image
Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo atahudhuria mkutano wa 20 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha. Utakumbuka hapo Mkutano Maalum wa 38 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifanyika Arusha kwa lengo lakujadili na kukubabaliana na agenda mbalimbali zitakazowasilishwa kwenyeMkutano huo wa leo. Mkutano huo utajadili agenda mbalimbali muhimu ambazo ni pamoja na ripoti ya utekelezaji wa maamuzi mbalimbali yaliyofikiwa na Baraza hilo kwenye vikao vilivyopita; taarifa kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, taarifa kuhusu masuala ya miundombinu, forodha na biashara na ripoti ya kamati ya utawala na fedha.

TBA watakiwa kukamilisha miradi kwa wakati

Image
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (rtd) Nicodemus Elias Mwangela amewataka Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) kukamilisha miradi ya ujenzi wanayo pewa ndani ya muda wa makubaliano ya mikataba. RC Mwangela ameyasema hayo jana wakati akishuhudia utiaji saini wa mikataba miwili ya ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Mkoa na ya Katibu Tawala Mkoa kati ya TBA na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe. “TBA mna sifa nzuri ya kujenga majengo ya serikali kwa kuzingatia ubora unaotakiwa na kwa gharama nafuu lakini kuna wakati kunakuwa na kusita katika kuwapa kazi kutokana na historia yenu ya kuchelewesha kukamilisha miradi mnayopewa ya ujenzi”, ameeleza Brig. Jen. (rtd) Mwangela. Ameongeza kuwa TBA wamechelewesha ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na ujenzi wa Hospitali ya Mji wa Tunduma hivyo ucheleweshaji huo usirudie katika mikataba hiyo miwili waliyopewa kwani hatasita kuvunja mikataba hiyo endapo wataonyesha ucheleweshaji. Naye Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Z. Kafulila ameishukuru serikali ya a...

Tundu Lissu amjibu Spika Ndugai kuhusu zile Tsh. Milioni 250

Image
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu amesema si kweli kwamba Bunge limemlipia fedha za matibabu kama livyoelezwa na Spika Job Ndugai. Tundu Lissu ambaye amekuwa akipatiwa matibabu nchini  Belgium  amesema Tsh. 250 Milioni ambazo Spika alieleza kuwa amepatiwa ni mshahara wake na posho ila sio kwa ajili ya matibabu. "Mil 207 ni mishahara na posho zangu za kibunge ambazo natakiwa kupata nikiwa mgonjwa au mzima kama yeye alivyopata akiwa anaumwa India, mil 43 ni michango ya wabunge waliyoitoa kwa hiari siku nimepigwa risasi," amesema Lissu. Hapo jana Spika alisema Spika hadi sasa Bunge limeshamlipa Mbunge huyo Tsh. Milioni 250 kwa ajili ya matibabu yake. katika kipindi cha maswali na majibu alisema hadi kufikia Desemba mwaka jana alikuwa amelipwa Tsh. Milioni 207, huku milioni 43 zikitolewa kama mchango. Huku akiongeza kuwa  mwanzo hakutaka kujibu kuhusu suala la matibabu ya Mbunge huyo kutokana alikuwa mgonjwa amelala kitandani na alikuwa amepitwa na ...

Kauli ya RC Makonda kwa Harmonize ilivyotikisa (+Video)

Image
Hapo jana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alikutana na wasanii wa muziki na filamu nchini ili kujua changamoto zao. Katika mkutano huo, RC Makonda aliibua suala kuhusu msanii wa WCB, Harmonize ambapo alitaka achunguzwe iwapo anatumia bangi. Hii ni baada ya muimbaji huyo kuchapisha picha kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha akivuta kitu kinachohisiwa kuwa ni bangi. "Huo moshi unavyotoka ni kama wa bangi, nimeongea na rafiki yangu Gavana wa Ghana pale anisaidie kumchunguza Harmonize, anatumia bangi au sigara na kama atakuwa anatumia bangi akitua hapa ni lokapu moja kwa moja," amesema. "Maana unavyojidhaminisha nivyo serikali itakudhamini, uwezi kuwa msanii anataka kubeba sura ya Tanzania, halafu tunapambana na dawa za kulevya halafu wewe (unafanya hivyo)," amesisitiza RC Makonda. Utakumbuka kuwa RC Makonda pia mlezi wa wasanii wote wa WCB akiwemo Harmonize. Wasanii wengine wa WCB ni pamoja na Diamond Platnumz, Mbosso, Rayvanny, Lava La...

IGP Sirro atuma kikosi Njombe kuwasaka wauaji

Image
Picha sio ya tukio Siku moja imepita tangu Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi amuagize IGP Simon Sirro kutuma kikosi maalumu cha kiintelinsia kuongeza nguvu katika uchunguzi wa watekaji na wauaji Wilayani Njombe, Hatimae hii leo kikosi hicho kimewasili Mkoani huko kikiongozwa na Kamisha wa operesheni na mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini Nsato Marijani. Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka akizungumza katika mkutano wa dharura na wananchi katika kituo kikuu cha mabasi mkoani humo akitamburisha kikosi hicho kilichosheheni wataalamu mbalimbali kutoka vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama nchini amewataka wananchi kutoa ushirikiano ili kuwabaini wahusika wamaovu hayo huku akidai hakuna mtu atakae achwa salama kama amehusika na mauaji. Katika mkutano huo pia Olesendeka amemuagiza Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe RPC Rennata Mzinga kumkamata mara moja aliyekuwa mratibu wa tiba mbadala na asilia mkoa wa Njombe Matias Gambishi ambaye pia ni afisa afya wa mkoa huo baad...

Timu nane kuingia dimbani katika mzunguko wa pili Ligi kuu bara

Image
Ligi Kuu Bara inaendelea Leo timu nane kuchuana kwenye Viwanja vinne kutafuta pointi tatu ikiwa ni mzunguko wa pili. Kagera Sugar watacheza leo na kikosi cha Tanzania Prisons Uwanja wa Kaitaba, KMC wapo mkoani Shinyanga watacheza na Stand United uwanja wa Kambarage. JKT Tanzania wataikaribisha Mwadui Uwanja wa Isamuhyo na Ruvu Shooting leo atakuwa kazini kumenyana na Mbeya City uwanja wa Mabatini.

MAGAZETI YA LEO 1/2/2019

Image

Wanaume kabla ya kuoa huangalia mwanamke mwenye sifa hizi

Image
Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha. Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri. Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa. Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa. 1. Mwenye mapenzi ya kweli. Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupat...

VIDEO: Kipa wa Biashara afunguka mazito, "Nilikuja Bongo kusaini Yanga"/ Naondoka Biashara (EXCLUSIVE)

Image
Kipa wa timu ya Biashara Nurdine Balora amefunguka mazito ambayo watu wengi walikuwa hawayafahamu. Kipa huyo ameweka wazi kuhusu matatizo yake na kocha wa klabu yake hiyo na sababu iliyompelekea kutolewa kwenye kipindi cha pili wakati wa mchezo wa ASFC dhidi ya Yanga. Balora pia ameweka wazi safari yake ya kuja Tanzania kwa mara ya kwanza ilikuwa ni kuja kusaini kuichezea Yanga lakini viongozi wa timu hiyo ndio walimuangusha na kupelekea kutimkia Biashara. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAU KUSUBSCRIBE

Faida nane (8) zitakanazo na matumizi ya pilipili mbuzi

Image
Watu wengi tumekuwa hatufahamu utumiaji wa pipilipili, hasa pilipili mbuzi. Naomba leo tuangalie kwa uchache faida hizo za pilipili mbuzi. 1. Pilipili inasaidia sana kusawazisha sukari kwenye damu. 2. Ulaji wa pilipili kunaweza kunawasaidia sana watu wanene (overweight) au wanao ugua ugonjwa wa kisukari. 3. Utafiti huo pia umeonyesha kwamba kawaida ya kula Pilipili kunaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti na kusawazisha insulini kwa 60%. baada ya kula chakula. 4. Pilipili husaidia kupunguza maumivu na uvimbe kwenye tezi na vilevile huwasaidia wagonjwa wa rheumatoid na arthritis kupata nafuu. Vile vile husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu moja ya mwili. 5. Pilipili usaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba kwa mafua, kuruhusu kupumua kwa urahisi zaidi! 6. Pilipili pia husaidia kupunguza upatikanaji wa saratani ya kwenye tumbo (Stomach Cancer) 7. Pilipili usaidia kuongezeka kwa kiwango cha metabolic, ambayo husaidia kuchoma mafuta, ulaji wa pilip...

Jinsi ya kufanya ili kupona majeraha mapema

Image
Hakuna mtu anayependa kupata majeraha au kuchelewa kupona majeraha. Kwa kuwa uhai na uzima wetu haupo mikononi mwetu, ni vyema tukafahamu kuwa kuna wakati tunaweza kuumia. Kwa kutambua hili karibu nikufahamishe mambo unayoweza kuyafanya ili kuharakisha kupona majeraha. 1. Kula vizuri Lishe bora ni muhimu wakati wote, lakini ni muhimu zaidi mara unapokuwa na majeraha. Ili uweze kupona majeraha mapema unahitaji ule matunda na vyakula vyenye protini, vitamini C, B12 pamoja na madini ya chuma kwa wingi. Vyakula na matunda hayo ni kama vile machungwa, mapapai, mayai, maziwa, samaki, maharage, n.k. Kwa kula vyakula hivi mwili utaweza kutibu majeraha kwa haraka zaidi. 2. Pumzika vya kutosha Kupumzika ni njia ya kuupa mwili nafasi ya kujijenga na kujitibu wakati wa majeraha. Kutokana na mtindo wa maisha au changamoto za kiuchumi, baadhi ya watu hawapati muda wa kupumzika wapatapo majeraha. Hivi leo utamkuta mtu akiendelea na shughuli zake huku akiwa na plasta, au bandeji bila hata k...

Epuka kufanya mambo haya wakati wa kulala

Image
Inasadikika ya kwamba mwanadamu hutumia masaa mengi sana kulala kuliko kufanya kazi, hautakiki kubisha kwani huo ndio ukweli. Pamaja na kusadikika huko kuna mambo tumekuwa tukiyafanya na kuona kama hayana madhara yoyote lakini ukweli ni kwamba kadri tabia hizo zinavyojirudia ndipo unakuja kugundua madhara yake baadae sana. Baadhi ya vitu ambavyo vipo katika maisha ya kila siku na watu wamekuwa wakijisahau kuyaepuka kabla ya kwenda kulala ni pamoja na ;- 1. Epuka kulala na simu yako karibu. Wanasayansi wanasema kuwa kionzi ya simu ni hatari sana wa afya ya ubongo ya mwanadamu ingawa wengi wetu tumekuwa na tabia ya kuweka simu karibu na vichwa kabisa wakati wa kulala, unashauri kuzima simu yako na kuaa nayo pembeni kutoka na usalama wa afya yako. 2. Usivae saa ya mkononi wakati wa kulala. Wanasayansi wanashauri kujitahidi kukumbuka kuuweka mwili wako kuwa na uhuru wakati wa kulaa, kitu chochote chenye kuufanya mwili wako kujihisi umebanwa sio kizuri, saa ya mkononi pia inaweza k...

Njia sahihi ya kujua wewe ni mtalamu wa kitu gani

Image
Katika haya maisha kila mmoja wetu amezaliwa ili kuweza kuwa mbobezi wa jambo fulani ila kutokana na ugumu wa maisha tunajikuta hatujia ni eneo gani ambalo sisi linatufanya tuweze kufanyia kazi , hivyo yafutayo ni ymambo ya msingi katika kujua ubobezi wako wa kazi upo katika eneo gani: Kitu gani kinakugusa? Kila mtu analo eneo la maisha linamvutia kulifuatilia kwa karibu. Kuna kitu ambacho ukikisikia kinazunguzwa mahali moyo wako unasisimka. Unapokuwa kwenye mazungumzo na watu wengine, masikio yako yanasikia kitu hicho hata kama watu wengine hawakisikii. Unanunua vitabu, unafuatilia televisheni na mitandao na karibu kila unachokifanya kinazunguka zaidi kwenye eneo hilo hilo. Unapoendelea kusoma hapa tayari kuna kitu kinakujia kichwani. Inawezekana ni matatizo fulani ya watu, hitaji fulani unalofikiri jamii yetu inalo au ubunifu fulani unaoamini bado jamii haijauona. Robert Green anasema, “Mambo yanayotugusa mara nyingi huwa hayabadiliki. Mtoto mdogo anajua kitu gani kinamgusa w...

Kamati ya Rufaa ya Maadili yatengua adhabu ya Meneja wa Simba

Image
Kamati ya Rufaa ya Maadili yatengua adhabu ya Meneja wa Simba Richard Robart iliyotolewa na kamati ya Rufaa ya TFF. Richard alifungiwa mwaka mmoja kujihusisha na Mpira na faini ya Shilingi Milioni nne.