Kauli ya RC Makonda kwa Harmonize ilivyotikisa (+Video)


Hapo jana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alikutana na wasanii wa muziki na filamu nchini ili kujua changamoto zao.

Katika mkutano huo, RC Makonda aliibua suala kuhusu msanii wa WCB, Harmonize ambapo alitaka achunguzwe iwapo anatumia bangi.

Hii ni baada ya muimbaji huyo kuchapisha picha kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha akivuta kitu kinachohisiwa kuwa ni bangi.

"Huo moshi unavyotoka ni kama wa bangi, nimeongea na rafiki yangu Gavana wa Ghana pale anisaidie kumchunguza Harmonize, anatumia bangi au sigara na kama atakuwa anatumia bangi akitua hapa ni lokapu moja kwa moja," amesema.

"Maana unavyojidhaminisha nivyo serikali itakudhamini, uwezi kuwa msanii anataka kubeba sura ya Tanzania, halafu tunapambana na dawa za kulevya halafu wewe (unafanya hivyo)," amesisitiza RC Makonda.

Utakumbuka kuwa RC Makonda pia mlezi wa wasanii wote wa WCB akiwemo Harmonize. Wasanii wengine wa WCB ni pamoja na Diamond Platnumz, Mbosso, Rayvanny, Lava Lava na Queen Darleen.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato