Tundu Lissu amjibu Spika Ndugai kuhusu zile Tsh. Milioni 250


Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu amesema si kweli kwamba Bunge limemlipia fedha za matibabu kama livyoelezwa na Spika Job Ndugai.

Tundu Lissu ambaye amekuwa akipatiwa matibabu nchini  Belgium  amesema Tsh. 250 Milioni ambazo Spika alieleza kuwa amepatiwa ni mshahara wake na posho ila sio kwa ajili ya matibabu.

"Mil 207 ni mishahara na posho zangu za kibunge ambazo natakiwa kupata nikiwa mgonjwa au mzima kama yeye alivyopata akiwa anaumwa India, mil 43 ni michango ya wabunge waliyoitoa kwa hiari siku nimepigwa risasi," amesema Lissu.

Hapo jana Spika alisema Spika hadi sasa Bunge limeshamlipa Mbunge huyo Tsh. Milioni 250 kwa ajili ya matibabu yake.

katika kipindi cha maswali na majibu alisema hadi kufikia Desemba mwaka jana alikuwa amelipwa Tsh. Milioni 207, huku milioni 43 zikitolewa kama mchango. Huku akiongeza kuwa  mwanzo hakutaka kujibu kuhusu suala la matibabu ya Mbunge huyo kutokana alikuwa mgonjwa amelala kitandani na alikuwa amepitwa na vitu vingi.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato