Njia sahihi ya kujua wewe ni mtalamu wa kitu gani

Katika haya maisha kila mmoja wetu amezaliwa ili kuweza kuwa mbobezi wa jambo fulani ila kutokana na ugumu wa maisha tunajikuta hatujia ni eneo gani ambalo sisi linatufanya tuweze kufanyia kazi , hivyo yafutayo ni ymambo ya msingi katika kujua ubobezi wako wa kazi upo katika eneo gani:

Kitu gani kinakugusa?
Kila mtu analo eneo la maisha linamvutia kulifuatilia kwa karibu. Kuna kitu ambacho ukikisikia kinazunguzwa mahali moyo wako unasisimka. Unapokuwa kwenye mazungumzo na watu wengine, masikio yako yanasikia kitu hicho hata kama watu wengine hawakisikii. Unanunua vitabu, unafuatilia televisheni na mitandao na karibu kila unachokifanya kinazunguka zaidi kwenye eneo hilo hilo.

Unapoendelea kusoma hapa tayari kuna kitu kinakujia kichwani. Inawezekana ni matatizo fulani ya watu, hitaji fulani unalofikiri jamii yetu inalo au ubunifu fulani unaoamini bado jamii haijauona.

Robert Green anasema, “Mambo yanayotugusa mara nyingi huwa hayabadiliki. Mtoto mdogo anajua kitu gani kinamgusa wakati mwingine vizuri zaidi kuliko mtu mzima. Usidharau mambo haya yanayokusisimua.”

Huenda unaguswa na masuala ya teknolojia; mfumo fulani wa maisha, imani au fikra katika jamii unazofikiri ungepewa nafasi ungezibadilisha. Chochote kile kinachogusa fikra zako, hicho ndicho kinachoweza kuwa wito wako. Ukifanya kazi zinazogusa eneo hilo unaweza kufanya vizuri zaidi.

Unajitambulisha na kitu gani?
Kwa kawaida, kuna vitu tukivifanya vikaleta matokeo fulani tunajisikia fahari. Kila mtu ana eneo lake akilifanya vizuri anajisikia kuridhika.  Kuna watu wanajisikia fahari wanapotetea haki za watu; wengine kufundisha; wengine uandishi; kubuni vitu vipya; kuongoza wengine; kushauri, kuendesha biashara, kutaja kwa uchache.

Kile kinachokuletea ufahari, mara nyingi, utapenda kujitambulisha nacho. Utatumia muda mwingi kukielewa kuliko unavyofanya kwenye maeneo mengine.

Nina rafiki yangu ambaye kila nikikutana naye lazima atazungumzia uharibifu wa mazingira. Dada huyu atazungumza kwa kirefu kwa nini anafikiri siasa za dunia zina athari kubwa kwa mazingira. Ukimsikiliza unaona wazi moyo wake uko kwenye mazingira. Hii ndiyo sifa ya wito wa mtu.

Jiulize, kitu gani ukikifanya vizuri unajisikia fahari? Je, watu wanakusifia na kukutambua kwa kitu gani? Ukiweza kuuoanisha uwezo huo na kazi unayoifanya itakuwa rahisi kupata mafanikio makubwa.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato