Rais Magufuli kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo
Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo atahudhuria mkutano wa 20 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
Utakumbuka hapo Mkutano Maalum wa 38 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifanyika Arusha kwa lengo lakujadili na kukubabaliana na agenda mbalimbali zitakazowasilishwa kwenyeMkutano huo wa leo.
Mkutano huo utajadili agenda mbalimbali muhimu ambazo ni pamoja na ripoti ya utekelezaji wa maamuzi mbalimbali yaliyofikiwa na Baraza hilo kwenye vikao vilivyopita; taarifa kutoka Ofisi ya
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, taarifa kuhusu masuala ya miundombinu, forodha na biashara na ripoti ya kamati ya utawala na fedha.
Comments
Post a Comment