Rais Magufuli ameongeza siku saba zaidi kwa watuhumiwa wa rushwa na uhujumu uchumi kuomba msamaha baada ya DPP kuomba aongezewe siku tatu kutokana na wengine kushindwa kukamilisha taratibu za kisheria kwa wakati. Rais Magufuli amesema hakutegemea kama watuhumiwa 467 wa kesi za uhujumu chumi wangeandika barua wakiomba wasamehewe, huku akimueleza DPP kuwa anafahamu kuna barua nyingine zimekwama kwenye ofisi zako za Mikoa, na kama kweli wapo waliokwamishwa kwa sababu ya umbali, "Natoa wito kwa Watanzania wenye tuhuma za uhujumu uchumi, wasiwe na wasiwasi kwamba ukishakiri basi kesho ndiyo ushahidi huo, siwezi nikafanya kazi ya kitoto namna hiyo, nimeshasema nimetoa msamaha ni msamaha kweli,hakuna msamaha wa majarbio au wa kumtega mtu, wasidanganywe" amesema. "Katika siku 7 wapo ambao walizuiliwa na Maofisa wa Magereza wakitaka hongo kidogo kwamba unatuachaje hapa ndani,Kamishina wa Magereza upo hapa mkafuatilie waliomba msamaha kwa DPP msiwakwamishe, hizi Bilioni 10...