Wanawake watakiwa kujitokeza kuwania nafasi za uongozi 2020



Na Thabit Madai, Zanzibar

Wanawake Nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya kuwania nafasi mbali mbali za uongozi katika Uchaguzi Mkuu ifikapo mwakani 2020.

 Wito huo umetolewa na Ali Haji Ubwa mwenyekiti wa kamati ya kushajihisha wanawake kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika wilaya ya kaskazini A Unguja.

 Ali Haji Ubwa alisema kuwa baadhi ya wanawake katika jamii hususani ya Zanzibar wamekuwa na muamko mdogo katika kugombania nafasi mbali mbali za uongozi nakubakia kuwa nyuma  katika masuala yamaendeleo.

Alisema wanawake kutokuwa katika nafasi mbali mbali za uongozi hupelekea kurudishwa nyuma kimaendeleo  na kuwa tegemezi katika jamii kutokana kuwa baadhi ya mambo yao kila siku yataendelea kuamuliwa na baadhi ya viongozi kwa maslahi yao.

 “Ukweli kwamba wakina mama (wanawake) wanakabiliwa na changamoto nyingi sana lakini  hakuna wa kuwasemea katika ngazi za maamuzi hivyo mimi kama mwenyekiti nawashauri kuwa wajitokeze katika kuwania nafasi mbali mbali za uongozi kwa yule anaehisi anaweza bila ya kurudi nyuma” alisema Ali Haji Ubwa.

Aliongeza kusema wanawake wanapokuwa mstari wa mbele katika kushika nafasi ya uongozi jamii haina budi kuwaunga mkono ili kushika nafasi hizo kwa lengo la kuzisemea changamoto zinazowaabili wanawake wenzao.

“Kuna baadhi yao huwa wana muamko wa kutaka kugombea lakini jamii inaonekana bado haijawa tayari katika kuwaunga mkono hawa wanawake kushika nafasi hizi, huwa wanarudishwa nyuma kwa kupewa kashfa mbali mbali na mwishoe wanarudi nyuma” alisema Ali haji Ubwa.

Alifafanua jambo hilo si zuri kwani linakosesha Taifa kupata viongozi ambao watakuwa mstari wa mbele kutetea maslahi ya wananwake Nchini.

Aidha alisema kuwa huu ni wakati wa kuwa karibu na wanawake hao kwa lengo la kuona yupi anafaa kushika nafasi ya uongozi na kuwa nae bega kwa bega hadi anafanikisha dhamira yake hiyo.

“Wakina mama huu si wakati wakusema wananwake hawawezi kuongoza, tunatakiwa kuwa nao na kuwachangua wale tunaohisi kwetu wanatufaa kutuongoza katika nafasi mbali mbali” alisema Ali haji ubwa.

Mapema Afisa kutoka Tume ya Taifa Uchaguzi ZEC akiongea na Muungwana Blog alisema kuwa wanawake Nchini huwa wana muamko wa kujitokeza kupiga kura na si kugombania nafasi za uongozi.

“Kwasasa tunatakiwa kuwapa elimu ya kutosha ya mpiga kura ili wengine wagombee na wengine wazidi kujitokeza kupiga kura na kuchagua wananwake wenzeo” alisema Afisa kutoka ZEC.

Aidha aliwahamisha kuwa ili uwe kiongozi kwa nafasi mbali mbali ya kugombea wanatakiwa kuwa na chama cha siasa na katika vyama hivyo apitishwe ndo atakuwa na sifa ya kugombea inapofika wakati.

Nae Msaidizi Afisa miradi na ufuatiliaji kutoka Tamwa Bi Sabrina alisema kuwa wao kama Tamwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakutete haki za wanawake wameandaa mpango maalumu wa kuwawezesha wanawake kushika nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu ifikapo mwakani.

“Programu hii kwa sasa tulianza kwa  kuwajengea uwezo wanaume wa mabadiliko ambao wao sasa watakuwa waelimishaji wakubwa kwa kina mama katika wilaya zao” alisema Sabrina.

Aidha alisema kuwa mpango huo wa kuwashijihisha wanawake kushika nafasi mbali mbali za uongozi kwa sasa utekelezwa katika wilaya zote za ungujaa Pemba.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato