Walimu wametakiwa kujiendeleza kielimu


Na Thabit Madai, Zanzibar

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Hassan Khatib Hassan amewataka walimu wa Shule za msingi katika Mkoa huo kujiendeleza kielimu ili kuongeza mbinu mbali mbali za ufunishaji nakuongeza ufaulu wanafunzi.


Wito huo ameutoa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya  walimu wa shule  za msingi ndani ya Mkoa Mjini Magharibi uliofanyika katika ukumbi wa kituo cha walimu Bububu Mjini Unguja.

Mafunzo hayo kwa walimu yameandaliwa na Taasisi ya Rafiki Elimu.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema suala la kujiendeleza kielimu kwa walimu litaongeza kasi ya mabadiliko na ukuwaji wa sekta ya elimu nchini hatua ambayo itaongeza wataalamu wa fani mbalimbali na kuwa na taifa lenye wasomi.

"Kazi hiyo ya ualimu ni kazi ambayo inahitaji mabadiliko hususan katika suala la kuongeza uwezo wa kitaalamu kujiendeleza ni jambo la msingi ili muweze kuwaanda vijana wetu wapende elimu na skuli na wapunguze mda wa kubaki nyumbani".

Aidha Hassan alisema  Serikali ya Mkoa huo itaendelea kusimamia kwa karibu maendeleo ya sekta ya elimu Mkoani humo ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya matokeo mazuri kwa wanafunzi wa ngazi zote.

"Suala la kuimarika kwa elimu katika nchi hii ni jambo la kipao mbele hata Mheshimiwa Rais suala la Afya na Elimu ni vitu ambavyo anavitilia mkazo sasa pamoja na hatua zilizofikiwa za kuimarikakwa  elimu basi na mimi nitaongeza kasi," Alisema  Hassan.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa alisema serikali ya Mapinduzi kupitia wizara ya elimu imekuwa ikiimarisha maendeleo ya sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya madarasa na vifaa vya kufundishia.

Nae Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi Rafiki Elimu Hussen Hassan alisema  Taasisi yao imekuwa ikijishuhulisha zaidi katika suala la elimu nchini ikiwemo utoaji wa mafunzo kwa walimu pamoja na ukarabati wa ujenzi wa madarasa ambapo madarsa 29 wamejenga  na 30 wamekarabati katika Mkoa Mjini Magharibi.

"Taasisi yetu imesajiliwa kisheria na tumekuwa tukifanya kazi kwa karibu na Serikali ya Mkoa Mjini Magharibi pamoja na Wizara ya elimu katika kusaidia sekta ya elimu nchini," alisema Mkurugenzi Hassan.

Mafunzo hayo yana lengo lakuwajengea uwezo walimu hao shule zote za msingi katika Mkoa wa Mjini Unguja.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato