Posts

Ndege ya kwanza ya Lufthansa yatua China

Image
Ndege ya Shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa, iliyobeba abiria 200 wengi wao wafanyakazi kutoka Ujerumani, imetua leo nchini China ikiwa ndege ya kwanza kutoka Ulaya kuanza safari zake nchini humo tangu ilipofuta mchakato wa kutoa visa kufuatia janga la virusi vya corona. China ilisimamisha kwa muda safari zake za kimataifa kuanzia mwishoni mwa mwezi Machi na kuweka marufuku ya wageni kuingia nchini humo hata kwa wale waliokuwa na vibali halali. Ndege ya Lufthansa kutoka Franfurt ilitua katika uwanja wa ndege wa Tianjin Kusini Mashariki mwa China. Kundi lililowasili nchini humo, likiwemo wafanyakazi wa kampuni za Ujerumani na familia zao lilipimwa ugonjwa wa COVID 19 baada ya kutua na wanapaswa kujiweka karantini kwa wiki mbili.

TPDC yawatoa hofu watumiaji wa gesi asilia majumbani

Image
Na Ahmad Mmow, Lindi. Watumiaji wa gesi asilia majumbani wametolewa hofu kuhusu usalama wao wakati wanatumia nishati hiyo. Watumiaji wametolewa hofu na mkurugenzi mtendaji wa shirika la petroli nchini( TPDC), Dkt James Mataragio kwenye hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa gesi asilia kwa wateja wa nishati ya kupikia majumbani. Hafla hiyo imefanyika leo katika mtaa wa Mnazimmoja, manispaa ya Lindi. Dkt Mataragio alisema gesi hiyo ni salama kuliko gesi ya mitungini(NLG), mafuta ya taa na kuni. Alisema usalama huo wa gesi asilia unatokana na gesi hiyo kuwa nyepesi kuliko hata hewa inayovutwa na binadamu. Kwahiyo ikitokea kuvuja kwanamna yoyote inatoweka na kupotea hewani. Hivyo kuondoa uwezekano wa kulipuka na kusababisha moto unaoweza kusababisha madhara kwa watumiaji. Alibainisha kwamba  usambazaji wa gesi hiyo ni salama. Kwani inasambazwa katika mgandamizo mdogo kwa njia ya bomba. " Hatahivyo shirika linaomba wananchi kufuata maelekez...

Singapore yathibitisha vifo 506 zaidi vya corona

Image
Wizara ya afya ya Singapore imesema imethibitisha visa vengine zaidi ya 506 vya virusi vya corona na kufikisha idadi jumla ya maambukizi kuwa elfu 34,366. Kulingana na taarifa ya wizara hiyo, wengi wa walioambukizwa ni wageni wanaoishi katika vyumba vidogo vya kupanga. Huku hayo yakiarifiwa Urusi imerekodi vifo 181 vinavyotokana na virusi hivyo vya corona ndani ya saa 24 zilizopita ikiwa ni idadi ndogo ikilinganishwa na vifo 232 vilivyoripotiwa siku iliyopita. Vifo nchini humo kwa sasa vimefikia 4,555. Hata hivyo maafisa wa afya wameripoti visa vipya zaidi ya elfu 8 vya maambukizi ya corona, na kwa sasa idadi jumla ya walioambukizwa virusi hivyo Urusi imefikia zaidi ya lakini 3 ikiwa ni taifa la tatu kuwa na idadi kubwa ya maambukizi baada ya Marekani na Brazil.

Ujerumani yasema Trump kutengana na WHO kutaathiri afya ya dunia

Image
Ujerumani imekasirishwa na uamuzi wa rais wa Marekani Donald Trump wa kukata mahusiano na shirika la afya ulimwenguni WHO ikiielezea hatua hiyo kuwa na muvunja moyo na inayorudisha nyuma afya ya dunia. "WHO inahitaji kufanyiwa mageuzi kama linataka kuleta maadiliko yoyote" aliandika Waziri wa afya wa Ujerumani Jens Spahn katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter, huku akisema Umoja wa Ulaya unapaswa kuchukuwa jukumu kubwa la kulisaidia shirika hilo kifedha na kusema hilo, ndilo litakuwa moja ya vipaumbele vya Ujerumani wakati itakapochukua urais wa kupokezana wa umoja huo Julai Mosi mwaka huu. Hapo jana Trump alisema anakata mahusiano ya Marekani na WHO anayoishutumu kwa kushindwa kuwajibika zaidi kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

Kansela Merkel kutohudhuria mkutano wa G7 Marekani

Image
Msemaji wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Steffen Seibert amesema kansela huyo, hatohudhuria mkutano wa viongozi wa kundi la Mataifa saba yenye nguvu zaidi kiuchumi duniani G7, ambao rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kuwa mwenyeji wa mkutano huo licha ya wasiwasi uliopo juu ya janga la virusi vya corona. Siebert amesema kutokana na hali halisi ya janga la corona ilivyo duniani, kansela hawezi kuthibitisha safari ya kutoka Ujerumani hadi Marekani kuhudhuria mkutano huo. Kansela Merkel aliye na miaka 65 ni miongoni mwa wazee katika kundi hilo la G7 baada ya Trump aliye na miaka 73 na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe aliye na miaka 65. Miaka yao inawaweka katika hatari zaidi iwapo wataambukizwa virusi vya corona. Ikulu ya Marekani imesema imeamua kuandaa mkutano huo wa ana kwa ana ili kuonesha namna mataifa makubwa yanavyorejea pole pole katika hali yake ya kawaida. Mkutano huo wa viongozi wa mataifa ya G7 ambayo ni Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan...

Waandamanaji wapuuza amri ya Polisi Marekani ya kutotoka nje

Image
Maelfu ya waandamanaji nchini Marekani wamepuuza amri ya kutotoka nje na kumiminika barabarani mjini Minneapolis kwa siku ya nne mfululizo, kupinga mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd chini ya mikono ya polisi. Maandamano hayo yamesambaa katika majimbo mengine zaidi nchini humo. Wizara ya ulinzi ikifuata maamgizo ya Rais Donald Trump, ililiamrisha jeshi kuweka tayari kikosi cha wanajeshi kitakachofika kwa haraka katika mji huo pindi kikihitajika, walisema maafisa watatu ambao hawakutaka kujulikana kwa majina. Hatua hiyo imefikiwa wakati vurugu zikienea katika miji mingine na kusababisha mwanamume mmoja kupigwa risasi mjini Detroit, magari ya polisi kuharibiwa Atlanta na mapambano kati ya polisi na waandamanji mjini New York. Afisa wa polisi mweupe Derek Chauvin, 44 aliyeweka goti lake kwa takriban dakika tisa shingoni mwa George Floyd Mmarekani mweusi alieaga dunia baadae tayari anakabiliwa na makosa ya jinai.

Wizara ya Mifugo yatoa vitendea kazi kuboresha uchunaji wa ngozi

Image
Wizara ya mifugo na uvuvi imetoa vitendeakazi vya mazao ya mifugo kwa wachunaji wa ngozi kwenye machiinjio yote ya mkoa wa Arusha kwa ajili ya kuongeza thamani na kuboresha uchunaji wa Ngozi. Akikabidhi vifaa hivyo kwa kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha kwa niaba ya wachunaji hao Mkurugenzi wa masoko na uzalishaji Felix Nandonde alisema kuwa kwa kipindi kirefu ngozi zimekuwa  zikiharibiwa ubora wake kwa matumizi ya vifaa visivyo na ubora. kwa mujibu wa Nandonde wizara ilitoa mafunzo ya siku moja kwa wachunaji wa ngozi mkoa wa Arusha ili kuboresha thamani ya Ngozi ikiwemo kutoa leseni kwa kila mchunaji na vifaa hivyo kwa lengo la kuongeza ubora kwenye kazi zao. Alivitaja vitendea kazi hivyo kuwa visu vya kisasa ambavyo vimetengezwa kwa teknolojia ya kisasa na vitatolewa bora kwa wachunaji wa mkoa wa Arusha na nchini kwa ujumla “Kwa kipindi kirefu sekta ya uchunaji nchini imekuwa ikionekana haina mwenyewe lakini sasa kupitia serikali ya awamu ya tano imeanza kutambulika k...