Waandamanaji wapuuza amri ya Polisi Marekani ya kutotoka nje
Maelfu ya waandamanaji nchini Marekani wamepuuza amri ya kutotoka nje na kumiminika barabarani mjini Minneapolis kwa siku ya nne mfululizo, kupinga mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd chini ya mikono ya polisi.
Maandamano hayo yamesambaa katika majimbo mengine zaidi nchini humo. Wizara ya ulinzi ikifuata maamgizo ya Rais Donald Trump, ililiamrisha jeshi kuweka tayari kikosi cha wanajeshi kitakachofika kwa haraka katika mji huo pindi kikihitajika, walisema maafisa watatu ambao hawakutaka kujulikana kwa majina.
Hatua hiyo imefikiwa wakati vurugu zikienea katika miji mingine na kusababisha mwanamume mmoja kupigwa risasi mjini Detroit, magari ya polisi kuharibiwa Atlanta na mapambano kati ya polisi na waandamanji mjini New York.
Afisa wa polisi mweupe Derek Chauvin, 44 aliyeweka goti lake kwa takriban dakika tisa shingoni mwa George Floyd Mmarekani mweusi alieaga dunia baadae tayari anakabiliwa na makosa ya jinai.

Comments
Post a Comment