Ndege ya kwanza ya Lufthansa yatua China

Ndege ya Shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa, iliyobeba abiria 200 wengi wao wafanyakazi kutoka Ujerumani, imetua leo nchini China ikiwa ndege ya kwanza kutoka Ulaya kuanza safari zake nchini humo tangu ilipofuta mchakato wa kutoa visa kufuatia janga la virusi vya corona.

China ilisimamisha kwa muda safari zake za kimataifa kuanzia mwishoni mwa mwezi Machi na kuweka marufuku ya wageni kuingia nchini humo hata kwa wale waliokuwa na vibali halali.

Ndege ya Lufthansa kutoka Franfurt ilitua katika uwanja wa ndege wa Tianjin Kusini Mashariki mwa China.

Kundi lililowasili nchini humo, likiwemo wafanyakazi wa kampuni za Ujerumani na familia zao lilipimwa ugonjwa wa COVID 19 baada ya kutua na wanapaswa kujiweka karantini kwa wiki mbili.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato