Wizara ya Mifugo yatoa vitendea kazi kuboresha uchunaji wa ngozi
Wizara ya mifugo na uvuvi imetoa vitendeakazi vya mazao ya mifugo kwa wachunaji wa ngozi kwenye machiinjio yote ya mkoa wa Arusha kwa ajili ya kuongeza thamani na kuboresha uchunaji wa Ngozi.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha kwa niaba ya wachunaji hao Mkurugenzi wa masoko na uzalishaji Felix Nandonde alisema kuwa kwa kipindi kirefu ngozi zimekuwa zikiharibiwa ubora wake kwa matumizi ya vifaa visivyo na ubora.
kwa mujibu wa Nandonde wizara ilitoa mafunzo ya siku moja kwa wachunaji wa ngozi mkoa wa Arusha ili kuboresha thamani ya Ngozi ikiwemo kutoa leseni kwa kila mchunaji na vifaa hivyo kwa lengo la kuongeza ubora kwenye kazi zao.
Alivitaja vitendea kazi hivyo kuwa visu vya kisasa ambavyo vimetengezwa kwa teknolojia ya kisasa na vitatolewa bora kwa wachunaji wa mkoa wa Arusha na nchini kwa ujumla
“Kwa kipindi kirefu sekta ya uchunaji nchini imekuwa ikionekana haina mwenyewe lakini sasa kupitia serikali ya awamu ya tano imeanza kutambulika kwa lengo la kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya mifugo”
Akiongea mara baada ya kupokea vifaa hivyo kaimu katibu tawala wa mkoa wa Arusha David Lyamongi aliipongeza wizara hiyo kwa kutoa mafunzo kwa wachunaji pamoja na vitendeakazi hivyo.
Aliongeza kuwa vitendeakazi hivyo vitawezesha mkoa huo kuzalisha ngozi zenye ubora wa hali ya juu na hivyo ngozi zitakuwa na thamani kubwa na masoko ya hali ya Juu.
Alisema kuwa mkoa wa Arusha ambao ni wa wafugaji vifaa hivyo vimekuja wakati muafaka kusaidia kuondokana na matumizi ya vifaa butu ambavyo vilikuwa vikitumika kuharibu ubora wa Ngozi na hivyo kuondoa thamani yake.

Comments
Post a Comment