Kansela Merkel kutohudhuria mkutano wa G7 Marekani

Msemaji wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Steffen Seibert amesema kansela huyo, hatohudhuria mkutano wa viongozi wa kundi la Mataifa saba yenye nguvu zaidi kiuchumi duniani G7, ambao rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kuwa mwenyeji wa mkutano huo licha ya wasiwasi uliopo juu ya janga la virusi vya corona.

Siebert amesema kutokana na hali halisi ya janga la corona ilivyo duniani, kansela hawezi kuthibitisha safari ya kutoka Ujerumani hadi Marekani kuhudhuria mkutano huo.

Kansela Merkel aliye na miaka 65 ni miongoni mwa wazee katika kundi hilo la G7 baada ya Trump aliye na miaka 73 na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe aliye na miaka 65.

Miaka yao inawaweka katika hatari zaidi iwapo wataambukizwa virusi vya corona. Ikulu ya Marekani imesema imeamua kuandaa mkutano huo wa ana kwa ana ili kuonesha namna mataifa makubwa yanavyorejea pole pole katika hali yake ya kawaida.

Mkutano huo wa viongozi wa mataifa ya G7 ambayo ni Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan na Mwenyeji Marekani, ulipangiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Juni katika makaazi yake Trump ya mapumziko ya Camp David jimboni Maryland.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato