Posts

Kauli ya Membe baada ya kufukuzwa uanachama CCM

Image
“Watanzania wenzangu nimepata habari ya kufukuzwa kwangu kutoka kwenye Chama changu cha CCM, simu zinamiminika hadi nashindwa kuzijibu, Tulieni! nitapata muda wa kuongea na wote muda si mrefu” - MEMBE

Breaking: Mzee Makamba asamehewa CCM

Image
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa CCM ikiongozwa na Mwenyekiti na Rais wa Tanzania Dkt Magufuli imemsamehe makosa yake ya kimaadili Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Yusuph Makamba, “Mzee Makamba ameandika barua na kuomba asamehewe”

Breaking: CCM yampa adhabu ya karipio Kinana

Image
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa CCM ikiongozwa na Mwenyekiti na Rais wa Tanzania Dkt Magufuli imempa adhabu ya karipio kali Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana  na hatokuwa na haki ya kugombea nafasi yoyote katika chama kwa kipindi cha miezi isiyopungua 18 kuanzia leo.

Breaking: CCM yamfukuza uanachama Membe

Image
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa CCM ikiongozwa na Mwenyekiti na Rais wa Tanzania Dkt Magufuli katika kikao cha kawaida cha Kamati hiyo kilichoketi leo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba, DSM imeazimia kumfukuza uanachama Bernard Membe.

NYUMBA MBILI ZINAUZWA ZIPO DAR

Image
HOUSE FOR SALE PRICE: Milion 55 SIZE PLOT SQM: 1300 DIRECTION: GOBA KWA AWAZI 4Bedroom 1bedroom is self CONTAINED SittingRoom  Diningi  Gypsum  Car parking  KITCHEN  Publictoilet   Call/WhatsApp 0713355443 / 0789279416 HOUSE FOR SALE ASKING PRICE: Milion 100 SIZE PLOT SQM: 400 DIRECTION: SINZA MAPAMBANO NEAR DOUBLE VIEW 3Bedroom 1bedroom is self CONTAINED SittingRoom  Diningi  Tiles  Gypsum  Car parking  Fenced  KITCHEN  Publictoilet  Umeme upo  Maji   Call/WhatsApp 0713355443 / 0789279416

China yahofia hatua ya kupeleka bata wala nzige, Pakistan

Image
Timu ya wataalamu nchini China imesema kwamba hatua yake ya kupeleka nchini Pakistan maelfu ya bata wanaoweza kuwala nzige waliovamia taifa hilo, huenda ikawa sio suluhisho bora, kwa kuwa mazingira ya nchi hiyo yanafanana na ya ukame wa jangwani ambayo hayawafai bata hao wanaopenda kuishi kwenye maji. Shirika moja la habari nchini China limeripoti jana kwamba bata 100,000 huenda wakapelekwa Pakistan, wakitokea jimbo la Zheijiang ili kuwala mabilioni ya nzige wanaosababisha uharibifu mkubwa wa mazao. Pakistan ilitangaza dharura ya kitaifa mapema mwezi huu, ikisema idadi ya nzige waliovamia sasa ni kubwa mno katika kipindi cha miongo miwili sasa. Kulingana na kituo hicho, bata hao watapelekwa kwanza kwenye maeneo yaliyoathirika zaidi. China iliwatumia bata hao, ilipovamia na nzige hao waharibifu wa mazao.

Luambano: CCM Kibaha Mjini yawaweka kitimoto wapiga debe wa wagombea

Image
Katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu ujao ,Chama Cha Mapinduzi (CCM),mjini Kibaha kimeanza kuwachukulia hatua baadhi ya wapambe wa wagombea ,wanaojipitisha kuwapigia debe wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi . Aidha chama hicho kimepiga marufuku wagombea wanaojipitisha na wapambe wao ,kuacha mara moja kufanya hivyo kwani wanakiuka taratibu na maadili ya chama. Akitoa taarifa kuhusiana na mkutano mkuu wa jimbo ,unaotarajia kufanyika march 2 mwaka huu,mjini Kibaha ,kwa lengo la mbunge wa jimbo hilo Silvestry Koka kueleza utekelezaji wa ilani, katibu wa CCM Kibaha Mjini ,Afidh Luambano alisema ,hadi sasa wamekaa vikao na kuwaonya wale waliosikika kujipitisha kuwanadi wagombea wao. “Hizo ni vurugu ,waache madiwani na mbunge aliyepo madarakani wafanye kazi na kumaliza muda wake ,waache kujipenyeza penyeza kwasasa sio muda wao”alifafanua Luambano. Luambano alieleza ,chama hicho kitaendelea kusimamia msingi na haki na wamejipanga kushinda kata zote na jimbo na Rais kati...