China yahofia hatua ya kupeleka bata wala nzige, Pakistan

Timu ya wataalamu nchini China imesema kwamba hatua yake ya kupeleka nchini Pakistan maelfu ya bata wanaoweza kuwala nzige waliovamia taifa hilo, huenda ikawa sio suluhisho bora, kwa kuwa mazingira ya nchi hiyo yanafanana na ya ukame wa jangwani ambayo hayawafai bata hao wanaopenda kuishi kwenye maji.

Shirika moja la habari nchini China limeripoti jana kwamba bata 100,000 huenda wakapelekwa Pakistan, wakitokea jimbo la Zheijiang ili kuwala mabilioni ya nzige wanaosababisha uharibifu mkubwa wa mazao.

Pakistan ilitangaza dharura ya kitaifa mapema mwezi huu, ikisema idadi ya nzige waliovamia sasa ni kubwa mno katika kipindi cha miongo miwili sasa. Kulingana na kituo hicho, bata hao watapelekwa kwanza kwenye maeneo yaliyoathirika zaidi.

China iliwatumia bata hao, ilipovamia na nzige hao waharibifu wa mazao.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato