Belarus yatishia kutumia risasi za moto dhidi ya waandamanaji
Mamlaka nchini Belarus jana zimetishia kutumia risasi za moto kuvunja maandamano dhidi ya rais Alexander Lukashenko huku mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wakikubaliana kumwekea vikwazo kiongozi huyo.
Akizungumza kwa njia ya video naibu waziri wa mambo ya ndani wa Belarus , Gennady Kazakevich amesema serikali haitowaondoa askari mitaani na iwapo maandamano hayatositishwa wanaweza kutumia risasi za moto .
Onyo hilo limetolewa baada ya vikosi vya serikali kutawanya kwa nguvu siku ya Jumapili maandamano ya kumpinga rais Lukashenko, hatua iliochochea Umoja wa Ulaya kufikia uamuzi wa kumwekea Lukashenko vikwazo.
Matumizi ya risasi za moto itakuwa ni hatua ya karibuni kabisa inayoonesha kuongezeka mvutano tangu raia wa Belarus walipoingia mitaani kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwezi Agosti na mateso wanayopitia mahabusu.
Comments
Post a Comment