Poland na Ukraine zatoa wito kwa Urusi kuhusu Crimea


Rais wa Poland Andrzej Duda na Rais wa Ukraine Vladimir Zelensky, wameitaka Urusi ikomeshe harakati zake za kutaka kujumuisha Crimea kama eneo lake kinyume cha sheria.

Kulingana na maelezo yaliyotolewa na ofisi ya rais wa Ukraine,  marais hao wawili walitoa wito kwa Urusi isitishe utekaji wa Crimea.

Duda, alibainisha kuunga mkono mipaka ya Poland na Ukraine, na kuweka msisitizo kuwa maeneo ya Donbas na Crimea yanapaswa kurejeshwa kwa Ukraine.

Duda pia alifahamisha kuwa vikwazo dhidi ya Urusi vinapaswa kuendelea hadi itakapositisha utekaji wa maeneo kinyume cha sheria, huku Zelensky akitoa shukrani kwa ushirikiano wa Poland katika suala la nchi yake na mwelekeo wa NATO.

Wakati huo huo, mazungumzo ya mkutano pia yalisisitiza umuhimu wa kulinda haki za jamii zilizokuwa na uchache katika nchi ya Ukraine na Poland.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato