Winga wa Yanga kuanza majukumu yake Novemba
WINGA Saidi Ntibazonkiza anayekipiga timu ya Taifa ya Burundi ambaye amesaini dili la mwaka mmoja na nusu ndani ya Klabu ya Yanga ataanza kutumika rasmi Novemba 15.
Kwa mujibu wa Injinia Hersi Said, Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Klabu ya Yanga amesema kuwa sababu kubwa ya kuanza kutumika Novemba 15 ni kutokana na kutimiza majuku ya timu yake ya Taifa ya Burundi.
Said alikuwa miongoni mwa wachezaji waliocheza Oktoba 11 Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Injinia Hersi amesema:"Ataanza kuutumikia mkataba wake tarehe 15 Novemba 2020 na ni mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
"Ataripoti kuitumikia klabu baada ya kumaliza majukumu ya timu ya taifa nchi yake inatarajiwa kucheza mechi ya pili tarehe 15 Novemba.
"Hivyo atakuwa ndani ya timu kwa nusu ya msimu huu na msimu ujao atakuwa msimu kamili na atamaliza kabisa kuitumikia timu ya Yanga," amesema.
Comments
Post a Comment