Mgombea udiwani kata ya Tandale aahidi Kujenga secondari ya Kata

 


Mgombea udiwani kata ya Tandale jimbo la kinondoni halmashauri ya wilaya ya kinondoni mkoani dar-es-salaam Kupitia chama cha ccm ndugu  Abdallah Azizi Saidi (Chief) ameahidi Kujenga shule ya secondary ya Kata.

 Aliyasema Hayo Jana wilayani kinondoni alipokuwa Akiomba kura kwa wananchi wa kata hiyo ya Tandale kupitia mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Tandale wilayani kinondoni Mbele ya Mgombea Ubunge Wa jimbo hilo la kinondoni Ndugu Abassi Tarimba.

Aidha Mgombea Huyo   amesema kuwa Atahakikisha Anatanua kituo cha Afya cha tandale,Atatoa Mikopo Isiyo na riba kubwa kwa kina mama,Atatoa Bima Za afya kwa watoto na kina mama,Atatoa msaada Wa kisheria pamoja na kusimamia ulinzi na usalama Wa Kata hiyo ya Tandale.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato