Posts
Belarus yatishia kutumia risasi za moto dhidi ya waandamanaji
- Get link
- X
- Other Apps
Mamlaka nchini Belarus jana zimetishia kutumia risasi za moto kuvunja maandamano dhidi ya rais Alexander Lukashenko huku mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wakikubaliana kumwekea vikwazo kiongozi huyo. Akizungumza kwa njia ya video naibu waziri wa mambo ya ndani wa Belarus , Gennady Kazakevich amesema serikali haitowaondoa askari mitaani na iwapo maandamano hayatositishwa wanaweza kutumia risasi za moto . Onyo hilo limetolewa baada ya vikosi vya serikali kutawanya kwa nguvu siku ya Jumapili maandamano ya kumpinga rais Lukashenko, hatua iliochochea Umoja wa Ulaya kufikia uamuzi wa kumwekea Lukashenko vikwazo. Matumizi ya risasi za moto itakuwa ni hatua ya karibuni kabisa inayoonesha kuongezeka mvutano tangu raia wa Belarus walipoingia mitaani kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwezi Agosti na mateso wanayopitia mahabusu.
SHULE YA MSINGI CHIPOLE SONGEA INAWATANGAZIA NAFASI ZA MASOMO
- Get link
- X
- Other Apps
Uongozi wa Shule ya msingi Chipole unawatangazia nafasi za kujiunga na masomo kwa Darasa la awali, i, ii, iii, v na vi kwa mwaka 2020 / 2021. Chipole Primary School ni shule ya bweni kwa wasichana na wavulana. inawalea watoto kimwili na kiroho, inafanya vizuri kitaaluma katika mitihani ya ndani, kata, wilaya, mkoa na kitaifa, Shule ipo Wilaya ya Songea kataya Magagura Mkoani Ruvuma. Shule ina mandhari nzuri ya kuvutia na tulivu inayo muwezesha mwanafunzi kujifunza na kufanya vizuri katika taaluma shule ina walimu wa kutosha wenye sifa thabiti za kitaaluma katika masomo yote. Standard four national assessment (sfna) -2019 results chipole primary school -ps1603003 waliosajiliwa : 29. waliofanya mtihani: 29. wastani wa shule: 287.1379 kundi la shule: watahiniwa pungufu ya 40 nafasi ya shule kwenye kundi lake katika halmashauri / manispaa: 2 kati ya 18 nafasi ya shule kwenye kundi l...
Winga wa Yanga kuanza majukumu yake Novemba
- Get link
- X
- Other Apps
WINGA Saidi Ntibazonkiza anayekipiga timu ya Taifa ya Burundi ambaye amesaini dili la mwaka mmoja na nusu ndani ya Klabu ya Yanga ataanza kutumika rasmi Novemba 15. Kwa mujibu wa Injinia Hersi Said, Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Klabu ya Yanga amesema kuwa sababu kubwa ya kuanza kutumika Novemba 15 ni kutokana na kutimiza majuku ya timu yake ya Taifa ya Burundi. Said alikuwa miongoni mwa wachezaji waliocheza Oktoba 11 Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Injinia Hersi amesema:"Ataanza kuutumikia mkataba wake tarehe 15 Novemba 2020 na ni mkataba wa mwaka mmoja na nusu. "Ataripoti kuitumikia klabu baada ya kumaliza majukumu ya timu ya taifa nchi yake inatarajiwa kucheza mechi ya pili tarehe 15 Novemba. "Hivyo atakuwa ndani ya timu kwa nusu ya msimu huu na msimu ujao atakuwa msimu kamili na atamaliza kabisa kuitumikia timu ya Yanga," amesema.
Poland na Ukraine zatoa wito kwa Urusi kuhusu Crimea
- Get link
- X
- Other Apps
Rais wa Poland Andrzej Duda na Rais wa Ukraine Vladimir Zelensky, wameitaka Urusi ikomeshe harakati zake za kutaka kujumuisha Crimea kama eneo lake kinyume cha sheria. Kulingana na maelezo yaliyotolewa na ofisi ya rais wa Ukraine, marais hao wawili walitoa wito kwa Urusi isitishe utekaji wa Crimea. Duda, alibainisha kuunga mkono mipaka ya Poland na Ukraine, na kuweka msisitizo kuwa maeneo ya Donbas na Crimea yanapaswa kurejeshwa kwa Ukraine. Duda pia alifahamisha kuwa vikwazo dhidi ya Urusi vinapaswa kuendelea hadi itakapositisha utekaji wa maeneo kinyume cha sheria, huku Zelensky akitoa shukrani kwa ushirikiano wa Poland katika suala la nchi yake na mwelekeo wa NATO. Wakati huo huo, mazungumzo ya mkutano pia yalisisitiza umuhimu wa kulinda haki za jamii zilizokuwa na uchache katika nchi ya Ukraine na Poland.
Mgombea udiwani kata ya Tandale aahidi Kujenga secondari ya Kata
- Get link
- X
- Other Apps
Mgombea udiwani kata ya Tandale jimbo la kinondoni halmashauri ya wilaya ya kinondoni mkoani dar-es-salaam Kupitia chama cha ccm ndugu Abdallah Azizi Saidi (Chief) ameahidi Kujenga shule ya secondary ya Kata. Aliyasema Hayo Jana wilayani kinondoni alipokuwa Akiomba kura kwa wananchi wa kata hiyo ya Tandale kupitia mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Tandale wilayani kinondoni Mbele ya Mgombea Ubunge Wa jimbo hilo la kinondoni Ndugu Abassi Tarimba. Aidha Mgombea Huyo amesema kuwa Atahakikisha Anatanua kituo cha Afya cha tandale,Atatoa Mikopo Isiyo na riba kubwa kwa kina mama,Atatoa Bima Za afya kwa watoto na kina mama,Atatoa msaada Wa kisheria pamoja na kusimamia ulinzi na usalama Wa Kata hiyo ya Tandale.