Posts

Wakili Mkuu wa Serikali azungumzia kesi ndege iliyokamatwa

Image
Maombi ya kupinga kushikiliwa kwa ndege ya Tanzania, Airbus nchini Afrika Kusini yanatarajiwa kusikilizwa leo na Mahakama Kuu nchini humo. Akizungumzia kesi hiyo Wakili Mkuu wa Serikali Msaidizi, DK Ally Possi alisema mawakili kutoka ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kupitia ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, watashirikiana  na mawakili wa Afrika Kusini katika maombi ya kupinga kushikiliwa kwa ndege hiyo. “Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wanasimamia suala hilo kuhakikisha ndege hiyo inaachiwa,”alisema. Ndege hiyo ilishikiliwa kutokana na maombi namba 28/994/2019 yaliyowasilishwa na mwombaji Hermanus Steyn kupitia ofisi ya uwakili ya Werksmans iliyopo nchini humo. Maombi hayo ya kusikilizwa upande mmoja yaliwalishwa Agosti 21 mwaka huu dhidi ya Serikali ya Tanzania, Uwanja Ndege wa Afrika Kusini, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Afrika Kusini, Kampuni ya Ndege Tanzania, Sibusis Nkabinde, Mr Kgomotso Molefi na Mr Patrick Sithole. Katika maombi hayo kuliambat...

Cristiano Ronaldo asema hana tatizo na Lionel Messi

Image
Mchezaji Cristiano Ronaldo anasema licha ya kuwa na upinzani mkubwa na Lionel Messi katika mpira wa miguu mahusiano yao yapo sawa yaani hawana tatizo. Ameongeza kuwa sio kitu rahisi kwa watu wawili wanaoshindana kusimama kwenye jukwaa moja katika kipindi kisichopungua miaka 15 huku kila mmoja wao akimpa hamasa mwenzake kushindana. Ronaldo pia amegusia jinsi ambavyo anaakosa kucheza Laliga ambapo wamekuwa na ushindani mkubwa na Messi amekiri pia licha ya ukaribu wao na kuwa na mahusiano mazuri hawakuwahi kujumuika pamoja kwenye chakula cha usiku akitaraji kufanya hivyo kwenye siku za usoni pengine.

Tanzania yatoa rai kwa Japan na Jumuiya za Kimataifa

Image
Tanzania imetoa rai kwa Jumuiya ya Kimataifa na Japan kuendelea kutafuta suluhu ya kudumu kwenye changamoto mbalimbalii ambazo bado zinajitokeza kwenye baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo ugaidi wa kimataifa, uhalifu, mabadiliko ya tabianchi, ukame, njaa na magonjwa sambamba na kujitolea kuchangia na kuwekeza kwenye miradi iliyobuniwa na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuboresha mazingira yaliyoharibiwa kutokana na uwepo wa kambi za Wakimbizi kwenye maeneo mbalimbali nchini. Rai hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu kuimarisha amani na usalama barani Afrika uliofanyika wakati wa Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD 7) uliomalizika leo tarehe 30 Agosti 2019 jijiji Yokohama, Japan. Waziri Mkuu amesema kuwa, miradi hiyo ambayo ni pamoja na kubadilishana teknolojia hususan kwenye maeneo ya mipakani na mifumo ya kutoa taarifa mapema kwa ajili ya kujikinga na majanga mbalimbali yanayo...

Chama cha Wafanyakazi Manyara chapata viongozi wapya

Image
Na. John Walter-Babati, Manyara Katika kuhakikisha wanafanya kazi zao katika Chama cha wafanyakazi wa serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Manyara wamefanya mkutano mkuu wa mwaka na kuchagua Viongozi katika nafasi mbalimbali ambao watakuwa wakiwasemea wengine katika nyanja mbalimbali. Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo msimamizi wa Uchaguzi Deodatus J. Munishi ambaye pia afisa kazi mkoa,aliwataja Viongozi waliochaguliwa katika nafasi mbalimbali kuwa ni Mjumbe kamati ya Ushauri wanawake mkoa kutoka wilaya ya Kiteto ambaye ni Rose Dismas Massay aliepata kura 117. Mjumbe wa kamati ya Utendaji mkoa Michael Faustin Yacob kura 83. Mjumbe Kamati tendaji Taifa amechaguliwa Devotha E. Mbonamasabo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Babati kitengo cha TEHAMA ambaye amepata  kura  90. Katibu Kamati ya Wanawake mkoa ni Julitha John Massay kura 80. Mjumbe mkutano mkuu TALGWU Taifa ni Isaack John Mgaya aliepata kura 85. Mwenyekiti wa TALGWU mkoa wa Manyara Dr.Martin John K...

Timu ya Jeshi zaendelea kutesa Mashindano ya Netibali Dodoma

Image
Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma Mashindano ya ligi daraja la kwanza Netibali ngazi ya taifa yameendelea kutimua vumbi ndani ya uwanja CCM Jamhuri jijini Dodoma, ambapo katika mchezo wa kwanza Jiji Tanga wameshinda kwa magoli 48, dhidi ya Jiji Dodoma. Mchezo wa pili JKT Makutopola wameshinda mabao 56, dhidi ya 24 ya Smart Queens, na JKT Mbweni wakashinda 60, dhidi ya 22 ya Coca cola Kwanza ya Dar es saalam, wakati Jeshi Stars wakishinda mabao 52, dhidi ya 31 ya Eagles. Na kwa upande wa wanaume Bright ya Dodoma wakashinda magoli 24, dhidi ya 19 ya Smart Boys ya Dar es saalam. Katibu wa CHANETA taifa Judith Ilunda ameiambia Muungwana Blog, kuwa  mashindano hayo yataendelea leo, august 30, saa mbili na nusu asubuhi kwa  TAMISEMI Dodoma dhidi ya Jiji Dodoma, Jiji Tanga dhidi ya JKT Makutupola. Wakati JKT Mbweni dhidi ya Eagles na mchana Jiji Arusha dhidi ya Jeshi Stars, na Coca cola kwanza watacheza na Smart Queens. Akataja timu zinazoshiriki mashindano hayo “Timu zinazosh...

Miradi ya mamilioni ya TASAF yazinduliwa Njombe

Image
Na Amiri kilagalila-Njombe Jumla ya miradi mikubwa minne ya jengo la utawala,nyumba za walimu nne na bweni la wanafunzi wa kike yenye thamani ya milioni 320 iliyotekelezwa na mfuko wa maendeleo ya jamii Tanzania TASAF imezinduliwa katika shule ya sekondari Mlowa iliyopo kata ya Mlowa mjini Makambako mkoani Njombe. Akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa miradi hiyo, Mkaguzi wa ndani wa TASAF Christopher Sanga kwa niaba ya mkurugenzi,amesema miradi hiyo ni miongoni mwa miradi mingi inayotekelezwa kwa sasa kwa mikoa miwili ya Arusha na Njombe licha ya kuwa mradi mkuu ukiwa ni kushughulikia kaya maskini. “Miradi hii ambayo inazinduliwa hapa ni miongoni mwa miradi mingi inayotekelezwa kwa kipindi hiki katika mikoa yetu miwili ya Arusha na Njombe,mradi mkuu unaoendelea wa Tasaf unajikita katika kushughulikia kaya maskini na huko tunakoenda tutatumia sana neno kaya washiriki katika mpango”alisema Christopher Sanga Sanga amesema utekelezaji wa miradi hiyo ni mpango muunganiko...

Simba SC waguswa na kifo cha aliyekuwa kiongozi wa TFF

Image
Uongozi wa Simba SC umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Makamu wa Pili wa Rais wa TFF.