Chama cha Wafanyakazi Manyara chapata viongozi wapya


Na. John Walter-Babati, Manyara

Katika kuhakikisha wanafanya kazi zao katika Chama cha wafanyakazi wa serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) Mkoa wa Manyara wamefanya mkutano mkuu wa mwaka na kuchagua Viongozi katika nafasi mbalimbali ambao watakuwa wakiwasemea wengine katika nyanja mbalimbali.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo msimamizi wa Uchaguzi Deodatus J. Munishi ambaye pia afisa kazi mkoa,aliwataja Viongozi waliochaguliwa katika nafasi mbalimbali kuwa ni Mjumbe kamati ya Ushauri wanawake mkoa kutoka wilaya ya Kiteto ambaye ni Rose Dismas Massay aliepata kura 117.

Mjumbe wa kamati ya Utendaji mkoa Michael Faustin Yacob kura 83.

Mjumbe Kamati tendaji Taifa amechaguliwa Devotha E. Mbonamasabo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Babati kitengo cha TEHAMA ambaye amepata  kura  90.

Katibu Kamati ya Wanawake mkoa ni Julitha John Massay kura 80.

Mjumbe mkutano mkuu TALGWU Taifa ni Isaack John Mgaya aliepata kura 85.

Mwenyekiti wa TALGWU mkoa wa Manyara Dr.Martin John Kongola amewapongeza waliochaguliwa huku akiwataka kuwa waaminifu katika kuwatumikia wafanyakazi wa serikali za Mitaa kwa kipindi cha miaka miwili iliyobaki.

Naye katibu wa TALGWU mkoa wa Manyara Ndulilah Pandauyaga alisisitiza ushirikiano kwa waliochaguliwa ili kukifanya chama hicho kiendelee kustawi.

Uchaguzi huo ulimalizika majira ya saa mbili usiku kutokana na wagombea kura zao kugongana na wengine kushindwa kufikia kiwango kinachohitajika hatua iliyomlazimu msimamizi wa uchaguzi huo kuamuru kura zirudiwe kupigwa upya ili wapatikane Viongozi watakaowatetea Wafanyakazi wa serikali za Mitaa katika ngazi ya wilaya,mkoa na hata Taifa.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato